Home Kitaifa MAADHIMISHO YA SIKU YA WANYAMAPORI DUNIANI

MAADHIMISHO YA SIKU YA WANYAMAPORI DUNIANI

Na Mercy Maimu

Waziri wa Mali Asili na Utalii  MOHAMED MCHENGERWA ametoa wito kwa wadau wote wa uhifadhi nchini kuendelea kushirikiana na Serikali kuhakikisha kuwa rasilimali za wanyamapori zinaendelea kuhifadhiwa kwa ajili ya kizazi cha sasa na kikazi kijacho.


MCHENGERWA ametoa rai hiyo leo wakati Dunia ikiadhimisha siku ya wanyamapori, ambapo kwa mwaka huu sherehe hizi zinakwenda sambamba na maadhimisho ya miaka 50 ya mkataba wa kimataifa  wa kudhibiti biashara ya wanyamapori na mimea iliyo hatarini kutoweka ambapo Tanzania ni mwanachama wa mkataba huo.


 Amesema wakati wanaadhimisha siku hii ni vizuri kukumbuka mchango wa Tanzania katika uhifadhi wa wanyamapori ambapo nchi imetenga asilimia 32.5 ya eneo lake kwa ajili ya uhifadhi wa wanyamapori linalojumuisha hifadhi za Taifa 22, mapori ya akiba 29, mapori tengefu 25,jumuiya ya hifadhi za jamii 38 pamoja na ardhioevu.

Kauli mbiu ya maadhimisho haya kwa mwaka huu ni Ushirikiano katika uhifadhi wa wanyamapori.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!