Home Kitaifa MAADHIMISHO YA SIKU YA USAFI DUNIANI YAANZA NA FUKWE ZA BAHARI YA...

MAADHIMISHO YA SIKU YA USAFI DUNIANI YAANZA NA FUKWE ZA BAHARI YA HINDI

Mkuu wa Wilaya ya kinondoni jijini Dar es salaam Saad Mtambule ameongoza Wananchi wa Kata ya Kunduchi na Mashirika yasiyoya kiserikali kufanya usafi katika maeneo ya fukwe ya bahari ya Hindi kwenye magofu ya Kunduchi ikiwa ni kushiriki Maadhimisho ya siku ya usafi wa mazingira duniani ambapo amesema dampo la kisasa kujengwa Magwepande ili kuendeleza usafi wa mazingira Wilayani humo.

Mheshimiwa Mtambule amesema ili kuhimalisha masuala ya kimazingira na uzoaji wa taka na kuzichakata limebainishwa eneo la kujenga dampo hilo la kisasa litajengwa huko Magwepande kwaajili ya kutupa taka za Manispaa ya Kinondoni jijini Dar es salaam.

Amesema kupitia dampo hiyo taka zinaenda kuwa mali kwa kuwa zinaenda kuzalisha ajira ambapo kupitia taka hizo inaweza kutengenezwa mbolea, gasi na bidhaa zingine mbalimbali.

“Kwa hiyo nitoe wito kwa wakazi wa Kinondoni kwa kuhakikisha wanakuwa sehemu ya kuhakikisha mazingira yetu yanakuwa safi na salama muda wote” amesema Mheshimiwa Mtambule.

Aidha kuhusu taadhari ya kuwepo mvua za elinino Mkuu huyo wa Wilaya ya Kinondoni amesema ni lazima kutunza mazingira kwa kuhakikisha mazingira yanakuwa safi kwa kuzibua mitalo ya maji machafu ili mvua hizo zikija maeneo yote yawe safi.

Nae Mkurugenzi Mkuu wa Lions club nchini Happiness Nkya amesema taasisi hiyo imeungana na dunia katika Maadhimisho hayo kwa kushiriki kufanya usafi wa mazingira huo wa fukwe ya bahari ya Hindi kwenye magofu ya Kunduchi.

Nkya amesema wanausafisha kwa kuondoa uchafu wote wa mazingira ili Wananchi waweze kufurahia maisha yao mazuri.Hatahivyo Mwanzilishi wa Taasisi ya Mazingira Plus Abdallah Mwikulu amesema wametumia siku ya tarehe 16 Septemba ambayo ni siku ya usafi wa mazingira duniani kutoa uelewa kwa jamii kuhusu nani wanaweza kupambana na taka ngumu kwenye mazingira yetu.

Amesema wametumia siku hiyo kuongeza hamasa ya kufanyia usafi hasa maeneo ya ufukwe kwani suala usafi na udhibiti wa taka kwenye fukwe linamuhusu kila mmoja.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!