Home Kitaifa MAADHIMISHO YA SIKU YA MILIKI UBUNIFU KUFANYIKA MEI 9 DAR ES SALAAM

MAADHIMISHO YA SIKU YA MILIKI UBUNIFU KUFANYIKA MEI 9 DAR ES SALAAM

Na Magrethy Katengu

Dar es salaam

WAKALA wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) mesema itahakikisha Taifa linafikia Maendeleo endelevu kwa kuthamini kulinda na kutambua Miliki Ubunifu unaofanywa na watu mbalimbali ikiwemo wanavyuo na wanasayansi kwa kuzitunza ili zitumike kuleta ufumbuzi wa changamoto zinazoikabili jamii.

Akizungumza na Waandishi wa Habari Jijini Dar es salaam Mei 8, 2023 Mkurugenzi wa Miliki Bunifu Loy Mhando Amesema maadhimisho hayo yalianzishwa na Shirika la miliki Ubunifu Duniani (WIPO) Ambapo huadhimishwa kidunia kila mwaka Aprili 26, kwa kuwa siku hiyo ni siku muhimu ya nchi kuadhimisha sikukuu ya Muungano hivyo kesho May 9 katika Hotel ya Johari rotana Maadhimisho hayo yanatarajiwa kufanyika huku mgeni rasmi akitarajiwa kuwa Waziri wa Viwanda na biashara Dkt. Ashatu Kijaji akiambatana na viongozi mbalimbali ambao watahudhuria maadhimisho akiwemo Naibu waziri utamaduni, sanaa na michezo, Hamis Mwinjuma.

“Maadhimisho ya siku ya Miliki Ubunifu Duniani huadhimishwa Aprili 26 kila mwaka lakini kwa hapa kwetu kutokana na Tarehe hiyo kuwa na jambo muhimu la kitaifa la kuazimisha Muungano sisi tunaazimisha siku tofauti ambapo mwaka huu tunaadhimishia tarehe 09/05/2024.” mesema Loy

Sanjari na hayo ameongeza kuwa katika maadhimisho hayo kutakuwa na matukio mbalimbali yatakayoambatana nayo ikiwemo mijadala kuhusu Miliki Ubunifu ambayo itahusu fursa, mafanikio na changamoto wanazokutana nazo nyanja nzima ya miliki Ubunifu.

Mkurugenzi Muhando Amesema katika siku hiyo watasaini hati za makubaliano ya ushirikiano katika eneo la Miliki Ubunifu baina ya BRELA, COSOTA na Chuo cha Mzumbe ikiwa ni njia ya kurasimisha ushirikiano uliopo baina ya Taasisi hizo katika kuhakikisha Miliki Ubunifu inaleta manufaa katika maendeleo ya kiichumi na teknolojia nchini na kukuza Ubunifu wa vijana

Pia Miliki Ubunifu ina tija kubwa kwa wabunifu ambapo inawapa ulinzi wa kumiliki bunifu zao na kuwasaidia katika kupata haki zao kupitia sheria zilizopo na endapo mtu yoyote ataingilia ama kutumia bunifu yake pasipo makubaliano na mmiliki lazima atawajibishwa au kutolea maelezo.

Mashirika ya kimataifa na kikanda ya Miliki Ubunifu yameongeza wigo wa ulinzi wa bunifu za wabunifu katika maeneo mbalimbali Duniani hususani kwa wabunifu wa kazi zinazovuka mipaka..

Wanawaalika wadau mbalimbali zikiwemo Taasisi zinazosimamia miliki ubunifu, Taasisi za umma pamoja na sekta binafasi katika Maadhimisho ya siku ya miliki ubunifu Duniani yatakayofanyika kesho Mei 09/2024 yakiongozwa na kauli mbiu isemayo “Miliki Ubunifu na Malengo ya Maendeleo endelevu kujenga mustakabali wa pamoja na kutumia ubunifu”

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!