Home Kitaifa Lugha ya Kiswahili ni fursa Watanzania tutumie kukuza uchumi wetu

Lugha ya Kiswahili ni fursa Watanzania tutumie kukuza uchumi wetu

Hayo yamesemwa na Balozi wa Tanzania nchini Italia Mahmoud Thabit Kombo wakati akizungumza Wadau wa Kiswahili, Wasanii na Wanafunzi kwenye Tamasha la Hamasa ya Shamrashamra ya Swahili festival lililofanyika katika Kijiji cha Makumbusho jijini Dar es salaam ambapo alikuwa Mgeni rasmi.

Kiswahili kimekubalika na kuzungumzwa katika mataifa mbalimbali duniani hivyo tukiinue kiendelee kukua zaidi duniani.

Amesema mataifa hayo yaliyokubali na kukizungumza Kiswahili wanauhifadhi wa utamaduni wetu wa mswahili.

“Nimeona kuna fursa nyingine tunazo lakini hatuzioni au hatuzitumii tutumie fursa ya Kiswahili , mswahili na tamaduni zake, chakula chake,Sanaa yake, kivazi chake, manukato yake na maisha yake kwasababu huo ndio utambulisho wenu nyinyi nyote”

Amesema “lugha ya Tanzania ni Kiswahili yaani makabila yote tumeunganishwa na lugha ya Kiswahili kwahiyo utambulisho Mkuu wa mtanzania ni Kiswahili, unapofungua mdomo wako popote duniani ni kiswahili”

Amesema “lugha ya Kiswahili imekuwa na kutambulika ni lugha rasmi ya kimataifa na Shirika la elimu sayansi utamaduni duniani UNESCO Sasa ni juu yetu kukipa kipaumbele kwa kuweka kiswahili chetu bendera juu maana tusipoweka sisi kitawekwa na mataifa mengine kwasababu ni fursa hiyo”

“Na fursa ikitokea lazima uitumie kwani goli likiwa wazi usipofunga wewe watafunga wengine kwani kiswahili kinazungumzwa na kimekubaliwa kimataifa na nchi zaidi ya 30 ambapo nchi ya kwanza ni Tanzania ya pili Kenya, ya tatu Uganda, ya NNE Rwanda, tano Burundi, sita Congo, saba Sudani ya kusini nane ni nchi za SADAC”

“Nchi zote za SADAC zimesaini lakini Afrika Kusini amekwenda hatua moja ya ziada ya kusaini kuifanya lugha rasmi kufundishwa kwasababu wanataka kuwa lugha moja wapo ya Mawasiliano ya kiofisi katika nchi yao na tayari watu wao wapo hapa nchini wanafundishwa ili wakawe Walimu”

Mkurugenzi wa Women Ubuntu Tanzania Dkt. Angella Gloria Bondo amesema wanahamasisha siku ya Tamasha la Kiswahili duniani tarehe 7 mwezi Julai kama ambavyo UNESCO walivyotoa azimio hilo mwaka 2021.

Dkt. Angella amesema wao Women Ubuntu Tanzania chini ya Balozi Mahmoud Thabit Kombo akiungana na Asas iliyoko kule Genivar Italia ya Shamrashamra association culture wanaoandaa Tamasha hilo ili hadi kufika mwezi huo jamii iwe na uelewa wa Tamasha hilo huko Genivar Italia chini ya ubalozi wa Tanzania.

“Tunachofanya sisi ni kuhamasisha kwamba siku hii inakuja na imeandaliwa huko nchini Italia ili kwamba na Watanzania waliopo kule wapate fursa ya kuona kuna jambo kubwa ambalo limendaliwa na ubalozi pamoja na Asas hiyo”

Afisa Elimu Kijiji cha Makumbusho Helmina Joseph unapozumza lugha ya Kiswahili unazungumzia utamaduni wa mtanzania.

Tanzania ambayo ina bahati sana kwani tuna makabila 120 ambayo yote yanazungumza lugha ya Kiswahili na ndio lugha inayotutambulisha na kutuunganisha.

“Kwahiyo Kijiji cha Makumbusho tunatoa wito kwa Watanzania kuthamini utamaduni wetu, lugha yetu ya Kiswahili kama ambavyo Balozi ameeleza”

+++++++

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!