Home Kitaifa LUDEWA YAKARIBISHA WAWEKEZAJI KWENYE SEKTA YA KILIMO.

LUDEWA YAKARIBISHA WAWEKEZAJI KWENYE SEKTA YA KILIMO.

Afisa Habari wa Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa Bwana Chrispin Kalinga amewahamasisha Watanzania kutembelea banda la Halmashauri hiyo kwenye maonesho ya Nanenane Kitaifa yanayoendelea kwenye Viwanja vya John Mwakangale Jijini Mbeya.

Akiongea kupitia Redio Uplands Fm Njombe Afisa Habari huyo alitumia nafasi hiyo kuwaeleza Watanzania kuwa Mkoa wa Njombe umejiandaa vyema kuwaonesha Watanzania fursa zilizopo kwenye Mkoa huo zikiwemo katika Kilimo cha Mahindi,Maharage,Kahawa,Korosho,Alizeti,Chai na Mazao mengine.

Sambamba na hayo alitumia nafasi hiyo kuwakaribisha Watanzania kwenda Wilaya ya Ludewa kuwekeza katika sekta ya Kilimo lakini pia katika sekta ya Utalii.

Aidha Afisa Habari huyo amesema Wilaya ya Ludewa imeshika nafasi ya pili Kitaifa kwa utoaji wa taarifa kwa Umma ikiwa ni pamoja na uhabarishaji wa taarifa za miradi mbalimbali pamoja mipango na mikakati inayotekelezwa kwenye Wilaya hiyo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!