Home Kitaifa LHRC WAPONGEZA CHAMA CHA MAPINDUZI KUKUBALI KATIBA MPYA

LHRC WAPONGEZA CHAMA CHA MAPINDUZI KUKUBALI KATIBA MPYA

Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) kimetoa mapendekezo manne kuhusu mchakato wa katiba mpya baada ya Chama cha Mapinduzi CCM kukubaliana kwenye mkutano wao wa Halmashauri Kuu.

Mapendekezo hayo yametolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa LHRC Anna Henga wakati wa mkutano wake na waandishi wa habari na kusema kuwa inapongeza maamuzi ya CCM kwa maamuzi hayo.

Pia LHRC imependekeza Serikali ipeleke mswada wa katiba, Serikali ipeleke mswada wa sheria. Serikali itumie rasimu ya pili ya Katiba ambayo inajulikana kama katiba ya Warioba na iendelee kufungua majadiliano na wananchi kupitia mikutano hata vyombo vya habari.

“31 Disemba 2010 aliyekuwa Rais wa Awamu ya nne wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete alitangaza mchakato wa Katiba wakati huo kulikuwa na kongamano la LHRC kauli mbiu ilikuwa KATIBA MPYA NI WAJIBU” amesema Henga

Sanjari na hayo Mkurugenzi wa ujengaji uwezo na uwajibikaji Felista Mauya amesema liundwe Bunge maalumu la Katiba litakalo fanikisha upatikanaji wa Katiba litakalo tumia rasimu ya pili.

Vilevile Afisa programu Maduhu William ameongezea kwa kusema mchakato wa Katiba ni jumuishi hivyo kuna watu wa makundi mbalimbali basi uwe shirikishi kwa watu wote.

“Katiba ni zaidi ya Dola, mchakato ili uwe hai lazima uwe rafiki ushirikishe makundi yote wakiwemo walemavu, wazee, vijana, wanafunzi kwa kufanya hivyo mchakato utakuwa rafiki kwa makundi yote ” amesema Maduhu.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!