Na Magrethy Katengu
Jeshi la Polisi Kikosi Cha Usalama barabarani limezuia leseni za Madereva 8,337 ambao hawana sifa ya kuwa ya kuwa na madaraja C na E na kufungia vyuo 161 vinavyotoa mafunzo ya udereva kwa kutokidhi vigezo na sifa..
Akizungumza na Waandishi wa habari Jijini Dar es salaam Mkuu wa Kikosi Cha Jeshi Polisi Kikosi cha usalama barabarani Kamanda Ramadhani Ng’anzi amesema Zoezi la uhakiki leseni za udereva kwa hiari lilianza Machi 1 hadi Julai 31 mwaka huu na kufahamu Madereva waliosajiliwa 1,725,473 ambapo Hadi Sasa leseni za madaraja C na E ambazo zimehakikiwa nchi nzima jumla ni 72,560 na kati ya hizo leseni 64323 na zimekutwa na sifa na madereva wake wamepewa barua ya uthibitisho na 8,237 zimezuiliwa kwa kukosa sifa.
“Uhakikii tuliifanya kwa shule na vyuo vinavyotoa mafunzo ya udereva na zoezi hili tulilianza Januari 2 mwaka huu na vyuo vilivyohakikiwa ni 297 vilivyokutwa na sifa stahiki 134 huku vyui 161 tukivifungia kutoa mafunzo ya udereva kwa kuwa havijakidhi sifa na vigezo” amesema Ng’anzi
Aidha Madereva wamefahamishwa. kuwa zoezi hilo la uhakiki ni endelevu kwa wale ambao walishindwa kufanyiwa uhakiki katika kipindi tajwa watawekewa utaratubu mzuri.