Home Kitaifa KWA MARA YA KWANZA SERIKALI SASA KUPATA 75% YA MAPATO YA MAFUTA...

KWA MARA YA KWANZA SERIKALI SASA KUPATA 75% YA MAPATO YA MAFUTA NA GESI

Waziri wa wizara ya Nishati January Makamba akiwa na wawakilishi kutoka TPDC, ARA petroleum na ndovu resources wakiwa katika zoezi la kusaini mkataba wa nyongeza wa uzalishaji na ugawanaji wa Mapato(PSA) kitalu Ruvuma hadi Mtwara

Baada ya miaka 12 Serikali ya Tanzania imesaini mkataba wa uzalishaji na ugawanaji mapato (PSA) kitalu cha RUVUMA – MTWARA.

Mkataba huu unaweka utaratibu wa serikali kupata zaidi mapato ,Kwa mara ya kwanza Serikali inapata kwenye Mapato ghafi (Gross) ambapo Kwenye huu mkataba serikali inapata 75%, ukilinganisha na huko nyuma ambapo ilikua inapata 68% kushuka chini.

Mara baada ya kusaini mkataba huo Waziri wa Nishati, January Makamba amesema “Siku hii ni kubwa na ya Kihistoria sababu Serikali inaenda kupata asilimia 75 ya Mapato Ghafi. 

Makamba akaongeza kuwa hii ndo tafsiri ya win-win na kazi hii imefanywa ndani ya mwaka mmoja.

Pia ametoa  Wito kwa wawekezaji kuwa na kasi ya haraka zaidi.

Nawataka tufanye kwa haraka ,Nataka ndani ya miezi 12 hadi 18 tuanze kutumia hii Gesi”.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!