Home Kitaifa KUWEPO kwa Mazingira Mazuri ya Kufundishia huwezesha Shule kufanya Vizuri

KUWEPO kwa Mazingira Mazuri ya Kufundishia huwezesha Shule kufanya Vizuri

KUWEPO kwa mazingira mazuri ya kufundishia katika shule zetu huwezesha wanafunzi kufanya vizuri katika mitihani yao mbalimbali.

Hayo yamebainishwa kwenye mahafali ya 15 kwa darasa la saba katika shule ya awali na msingi Mzigu iliyopo Jijini Mwanza na wadau mbalimbali wa elimu.

Mwakilishi wa Afisa Elimu Mkoani Mwanza Jovitha Mombeki aliipongeza shule hiyo kwa kuwa mara zote ikifanya vizuri kwenye mitihani yake ya kiwilaya,kimkoa na kitaifa.

Alisema serikali inathamini mchango wa shule binafsi katika utoaji wa elimu kwa watanzania na kutaka jitihada hizo ziendelezwe ili wazazi na walezi wafurahie matokeo ya watoto wao.

“Naamini ushindi wenu unatokana na namna mnavyo jali na kuweka miundombinu rafiki ya ufundishaji na motisha kwa walimu wenu” alisema Mombeki.

Mwalimu Mkuu wa shule hiyo Mathew Ferguson alisema kuwa kwa miaka 14 mfululizo hakuna mwanafunzi aliyeshindwa mtihani wa kuingia kidato cha kwanza.

Alisema mwaka 2018 shule hiyo kwenye mtihani wa taifa kiwilaya ilikuwa ya kwanza, kimkoa ya tatu na kitaifa ya 16 huku mwaka 2019 wakawa wa pili kiwilaya, kimkoa ya sita na kitaifa ya 20.

Ferguson aliongeza kusema kuwa mwaka 2020 walikuwa wa saba kiwilaya,18 kimkoa na kitaifa ya 50 huku 2021 kiwilaya wakawa wa nne, saba kimkoa na 63 kitaifa.

Aliongeza kusema kuwa mwaka 2022 shule hiyo ilipata ufaulu wa daraja A Bora ambapo wanafunzi 10 walichaguliwa kwenda shule maalumu.

Meneja wa shule hiyo Tamila John alisema kuwepo kwa mazingira mazuri ya kujifunza na kufundishia kuwa vitu pekee vinavyowafanya kufanya vizuri katika mitihani yao.

Alisema kuwepo kwa vifaa vya kutosha vya kufundishia, mazoezi ya kutosha na kuwa motisha walimu na watumishi kuwa ni siri ya kuendelea kuwa na matokeo bora muda wote.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!