Home Kitaifa KUTOKUSIMAMA KWENYE VIVUKO KUNACHANGIA AJALI

KUTOKUSIMAMA KWENYE VIVUKO KUNACHANGIA AJALI

Mkuu wa Dawati la elimu ya usalama barabarani Tanzania Kamishina Msaidizi wa Polisi, Michael Deceli amewataka madereva wa vyombo vya moto kuzingatia alama za barabarani ili kupunguza ajali kwa watumiaji wengine wa barabara.

Akizungumza jana Mei 08, 2024 baada ya kuhitimisha utoaji wa elimu ya uvukaji wa barabara kwenye vivuko vya waenda kwa miguu kwa wanafunzi wa shule ya msingi Misugusugu Wilaya ya Kibaha Mkoani Pwani Deceli amesema kumekuwepo na baadhi ya madereva wa vyombo vya moto wakiwemo madereva wa serikali kutokusimama kwenye vivuko vya waenda kwa miguu na kupelekea ajali katika baadhi ya maeneo.

“Suala la kuheshimu alama za barabarani ni la kila dereva anayeendesha chombo cha moto, Sheria haijabagua madereva wa kuziheshimu alama hizo na wengine kutokuheshimu”.

Kadhalika, Deceli amewataka madereva walioweka magari yao ving’ora pasipo kuwa na kibali cha Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi kuondoa mara moja na wale watakao kamatwa wakiwa hawana vibali hivyo watachukuliwa hatua za kisheria.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!