Home Kitaifa KUPITIKA KWA BARABARA ZINAZOSIMAMIWA NA TANROADS MARA KIPINDI CHA MVUA WANANCHI WAPONGEZA

KUPITIKA KWA BARABARA ZINAZOSIMAMIWA NA TANROADS MARA KIPINDI CHA MVUA WANANCHI WAPONGEZA

Na Shonari Binda-Musoma

WANANCHI kwenye maeneo mbalimbali ya mkoa wa Mara wameipongeza Tanroads mkoa wa Mara kwa usimamizi mzuri wa barabara.

Kutokana na usimamizi huo umepelekea barabara hizo kupitika katika kipindi hiki cha mvua na kuendelea kufanya shughuli za kiuchumi

Wakizungumza na Mzawa Blog kwa nyakati tofauti kwenye maeneo yao wamesema bila usimamizi mzuri na ufatiliaji barabara hizo zisinge pitika kwenye kipindi hiki.

Wambura Mwita mkazi wa Tarime amesema licha ya uwepo wa mvua nyingi shughuli kiuchumi zimekuwa zikiendelea kutokana na barabara kupitika.

Amesema yapo maeneo ambayo wamekuwa wakiyaona kwenye vyombo vya habari yakishindwa kupitika kutokana na mvua zinazoendelea.

Marwa amesema Tanroads mkoa wa Mara wamekuwa wakionekana maeneo yenye changamoto na kufanya utatuzi wa haraka na hakuna barabara hadi sasa iliyoshindwa kupitika.

Mkazi wa Mugumu Serengeti Mwita Warioba mjasiliamali wa kuuza ndizi kutoka Tarime amesema hajasimama biashara kutokana na barabara kufungwa kwa sababu ya mvua.

Amempongeza meneja wa Tanroads Mara pamoja na wasaidizi wake kwa kazi mzuri wanayofanya na kupelekea barabara kupitika kwa wakati wote.

Tunampongeza meneja wa Tanroads mkoa wa Mara na watumishi wote kwa uwajibikaji wao kwenye majukumu ya kusimamia barabara.

Kila mmoja ameshuhudia kwenye kipindi hiki cha mvua hakuna barabara iliyofungwa na shughuli zetu za kiuchumi zimekuwa zikiendelea“,amesema Warioba.

Hivi karibuni katika kikao cha bodi ya barabara mkuu wa mkoa wa Mara Said Mtanda alisema hakuna athari yoyote iliyotokea kutokana na athari ya mvua na hakuna barabara iliyofungwa.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!