Na John Mapepele, Birmingham
Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo. Mhe Mohamed Mchengerwa ameitembelea timu ya wachezaji wa Tanzania inayoshiriki mashindano ya Jumuiya ya Madola Birmingham nchini Uingereza na kuitaka kupambana kufa na kupona ili kurejea na medali.
Mhe. Mchengerwa ameyasema haya leo Julai 27, 2022 kwenye kambi ya timu hiyo huku akisisitiza kuwa watanzania wakiongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Mhe Samia Suluhu Hassan wana matumaini makubwa na timu hiyo hivyo hawana budi kulinda heshima kubwa waliyopewa na taifa kwa ujumla.
“Nawaomba tangulizeni uzalendo ili tuweze kushinda, hii ni vita tunahitaji kupambana bila kujali idadi yetu wala kitu chochote. Tutashinda.” Amesisitiza Mhe. Mchengerwa
Aidha, amesema dhamira ya Serikali kwa sasa ni kuinua na kuendeleza michezo kwa kuwa michezo ni chanzo. Ha ajira na uchumi kwa taifa
” kwa kutambua hilo ndiyo maana kwa mara ya kwanza Serikali imeamua kutoa fedha nyingi kwa wachezaji watakaopata medali za dhahabu dola za kimarekani 10,000, shaba 7500 na fedha 5000 bado zawadi za jumla” amesisitiza Mhe. Mchengerwa.
Pia ametumia tukio hilo kutoa pongezi kwa timu ya wanaume na wanawake ya KABBADI kwa kufuzu kuingia kwenye mashindano ya kombe la Dunia yatakayofanyika Oktoba mwaka huu nchini India.
Mhe Mchengerwa ameongozana na Mhe. Musa Sima Mjumbe wa Kamati ya Bunge inayosimamia wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo na ndugu Saidi Yakubu Naibu Katibu Mkuu.