Na Scolastica Msewa, Kibaha.
Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Zanzibar Riziki Pembe Juma amesema serikali imeweka kipaumbele kikubwa katika kumsaidia watoto wa kike ili waweze kufikia malengo yao ya kimaendeleo hasa kwa kuhimalisha elimu ya mtoto wa kike nchini.
Amesema hayo wakati akifunga mkutano Mkuu wa tatu wa Mwaka wa Mtandao wa Vijana Wanawake Viongozi barani Afrika uliofanyika katika Shule ya Uongozi ya Mwalimu Julias Nyerere iliyopo Kibaha mkoani Pwani ambapo wawakirishi kutoka nchi 16 wamehudhuria.
Alisema serikali inawapa hamasa zaidi vijana hao wanawake viongozi kwa inazifikia changamoto zinazowakabili na kuona namna gani inaweza kupambana nazo kwani vijana hao wana nafasi kubwa na safari ndefu ya katika kutimiza ndoto zao za maendeleo.
Alisema katika mkutano huo mambo mbalimbali yamezungumzwa ikiwa ni pamoja na udhibiti udhalilishaji wa wanawake na watoto, na masuala gani ya kuwainua wanawake kiuchumi na masuala mengine ya wanawake kushiriki katika vyombo vya maamuzi na masuala mengine.
Alisema serikali imeweka kipaumbele kikubwa kwa mtoto mwanamke kwa kuona anafikia malengo yake kwa kuhimalisha masuala ya elimu ili asome vizuri katika mazingira mazuri na salama mjini na vijijini ili kuona kwamba mtoto wa kike hatembei masafa marefu katika kupata elimu”
“Hiyo yote ni katika kuwapunguzia changamoto mbalimbali za kesi za udhalilishaji ambazo zilikuwa zikiwakumba katika miaka ya nyuma”
“Lakini pia vile vile katika kuwashirikisha vijana katika vyombo vya maamuzi kama wanawake vijana ambao wameingia katika nafasi za uwakirishi kwenye bunge na baraza la uwakirishi la serikali ya mapinduzi ya Zanzibar na katika selikalikuna viongozi wanawake vijana wengi wamo”
“Marais wetu wanachagua viongozi wanawake vijana kwamba sisi Tanzania katika masuala ya kutoa kipaumbele kwa vijana sisi tumetangulia kufanya vizuri hata katika kuwawezesha wanawake kiuchumi serikali zetu zimetoa fursa ya mikopo isiyo na riba kwa vijana hawa kupitia mikopo ya halmashauri ambapo asilimia nne wanapewa wanawake na vijana”
“Lengo likiwa ni kuwahimalisha wanawake kiuchumi ili awezekusimama na kujitegemea kiuchumi na kwa upande wa kijamii pia sera zetu zimekuwa zikiwezesha jamii ya wanawake ili kuwanusulu vijana hawa wanawake katika masuala ya kupinga vitendo vya uzalilishaji wa wanawake kijinsia”
Naye Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu Ummy Nderiananga amewataka wanawake vijana wanaendelea kuwa imara kwa kuendelea kushiriki kikamilifu kwenye maeneo mbalimbali ya uongozi ikiwa ni pamoja na maeneo ya ngazi za maamuzi ili taifa liendelee kupiga hatua za maendeleo.
Akizungumzia uongozi wa Rais Dkt. Samia kwa jinsi ulivyofaraja na msaada kwa kundi la wanawake nchini Ummy alisema wanawake wanavutiwa na kufarijika na uongozi wake hivyo amewataka kuendelea kutoa ushirikiano kwa Rais huyo ili taifa liendelee kunufaika na uongozi wake.
Naye Mkuu wa Idara ya Uchumi na Mabadiliko ya kijamii barani Afrika wa Mtandao wa Vijana Wanawake Viongozi barani Afrika Emmanuela Mtatifikolo amesema mkutano huo wa tatu umekutanisha vijana viongozi wanawake kutoka nchi 16 wa bara la Afrika lengo kuu likiwa ni kupeana taarifa ya kazi walizofanya kwa miaka hiyo mitatu tangu kuanzishwa kwa mtandao huo na kusherekea miaka mitatu ya kuundwa kwa mtandao huo.
Alisema pia wamekutana ili kujadili changamoto zote ambazo zinazowakumba vijana viongozi wanawake kwenye kada mbalimbali ambazo wapo tayari kufanya mabadiliko makubwa katika jamii zao.
Alizitaja baadhi ya sekta ambazo wanataka mabadiliko kuwa ni pamoja na katika sekta ya kilimo, ufugaji, biashara ndogo ndogo, biashara kubwa, shughuli za madini na waliopo katika mashirika yasiyoyakiserikali ikiwa ni pamoja na watu wa aina zote.
“Tunamaelekezo ya kwamba kwenye maendeleo hakuna kumuacha mwanamke yoyote nyuma hivyo hata katika mtandao huu makubaliano tuliyonayo ni kwamba hakuna kumuacha mwanamke yoyote nyuma” alisema Emmanuela.
“Tumejiwekea malengo sasa kwa miaka inayofuata tutashughulika na masuala ya kupinga ukatili wa kijinsia kwenye jamii, mazingira, kumjenga mwanamke kiuchumi, kusaidiana, kutengeneza mtandao wa kibiashara ndani ya nchi za Afrika kati yetu sisi wanawake na kujengeana uwezo pia kwa wale wanaotaka kuanzisha makampuni, mashirika yasiyokuwa yakiserikali, ufugaji, uvuvi tutaendelea kubadilishana uzoefu pamoja na kupeana fursa ambazo zinazopatikana kwenye maeneo yetu ilikumjenga mwanamke pia kiuchumi” alisema Emmanuela