Home Kitaifa KUMI NA MOJA WANAHOJIWA NA TAKUKURU KWA TUHUMA ZA KUJIGAWIA VYAKULA VYA...

KUMI NA MOJA WANAHOJIWA NA TAKUKURU KWA TUHUMA ZA KUJIGAWIA VYAKULA VYA WAATHIRIKA WA MAFURIKO RUFIJI

Na Scolastica Msewa, Rufiji
Watendaji wa kata na kijiji pamoja na vibarua tisa waliokua wakifanya shughuli ya kupokea misaada kwaajili ya waliokumbwa na mafuriko wilayani Rufiji wanashikiliwa na Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa TAKUKURU kwa tuhuma za kujihusisha na wizi wa vyakula vya misaada inayotolewa na serikali kwa kushirikiana na Wahisani mbalimbali kwaajili ya kuwapatia waliokumbwa na mafuriko wilayani humo.

Akielezea tukio hilo linalowakabili watuhumiwa hao Mwenyekiti wa kamati ya maafa ambae pia ni Mkuu wa Wilaya ya Rufiji Meja EDWARD GOWELE amesema tayari watuhumiwa hao wanashikiliwa na taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa TAKUKURU kwaajili ya mahojiano zaidi huku akiwaonya wanaopewa dhamana ya kusimamia misaada hiyo kutojihusisha kwa namna yoyote ile kujichukulia au kuiba misaada hiyo na atakaebainika serikali haitosita kumchukulia hatua kali za kinidhamu.

Alisema wapo Mtendaji wa Kata na Kijiji ambao walikiuka miongozo kwa kutoa chakula au kwa kujigawia chakula nje ya utaratibu huku wakijua wazi wao sio waathirika wa mafuriko na tayari wamechukuliwa hatua ambapo TAKUKURU wanaendelea na uchunguzi dhidi yao.

“Pia wapo vijana ambao tunawatumia kwa kazi za vibarua wa kushusha mizigo nao walifanya hivyo TAKUKURU waliwakamata vijana 9 ambapo wanaendelea kushughulika nao kwa mujibu wa sheria” alisema Meja Gowele.

Aidha Meja Gowele alitoka wito kwa Watendaji na wasiostahili kupata chakula wasichukue chakula ambacho hawajapewa.

“Lazima tufuate taratibu na miongoni ambayo tumepewa katika shughuli nzima ya ugawaji wa hiki chakula sio Watumishi wa umma ambao tunasimamia hiyo Kazi na Wananchi kwa ujumla kwani chakula kingi kinacholetwa ndani ya wilaya na hao wanaoleta chakula matarajio yao kiende kwa waliolengwa na sio kwa Kila mtu na kisichukuliwe nje ya utaratibu” alisema Gowele.

“Sasa wapo ambao wameshaanza kufanya vitendo vya namna hiyo na sisi Wilaya tumeanza kuchukua hatua, wapo Watendaji wanaojihusisha na hayo mambo licha ya kupewa maelekezo mahususi na serikali lakini wamekuwa wakikiuka”

“Pia wapo vijana wengi ambao wanafanya kazi ya kutusaidia kushusha mizigo lakini tunawalipa na kama tunawalipa hawastahili kupewa chakula hicho cha msaada kwasababu chakula hiki kimelenga moja kwa Moja kwenda kuwasaidia wale waliokubwa na changamoto”

“Maana tuna watu kwenye makambi hawana makazi kabisa wapo kwenye kambi ya pale Chumbi ambako kinahitajika chakula, malazi, huduma za kiafya na shughuli zingine za kijamii zinazoendelea pale”

“Tunaomba misaada kutoka kwa watu mbalimbali sisi tunawajibu wa kusimamia kwahiyo tusingependa kusikia Kuna mtu anatia mkono ambaye hastahili kupewa na tayari tumeshaanza kuchukua hatua kwa wale ambao tumewakamata eitha walijaribu kwa namna Moja au nyingine kufanya vitendo ambavyo havistahili au havipo kwenye muongozo”

“Nitoe wito kwa Watendaji wote na kwa Wananchi wote tuwe na Moyo wa huruma kwa kipindi hiki kwa ndugu zetu ambao wana changamoto kubwa maana sisi tumepewa dhamana ni lazima tuzingatie miongozo tuliyopewa katika kuwahudumia Watanzania”

“Watu ambao hawastahili kupata chakula wasipate chakula aidha kwa kupewa au kwa kuiba na atakayefanya hivyo sisi hatutamuonea huruma hutachukua hatua kwa kadri alivyofanya kitendo hicho”

Alisema bado serikali inaendelea kupeleka misaada mikubwa wilayani humo ya chakula na vifaa kwaajili ya Waathirika wa mafuriko ya Mto Rufiji maana ni watu wengi wameathirika kwani zaidi ya Watu 89000 Walioathirika, kaya 23060 na baadhi ya makazi yameathirika.

“Tunao watu wameathirika sana kwa maana ya hali duni wengine wamewekwa kwenye makambi na wapo waliochukuliwa na ndugu, jamaa na marafiki zao lakini tunawajibu wa kuhakikisha kwamba tunasimamia ili waweze kupata msaada ambao serikali imekusudia”.
+++++++

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!