Naibu katibu mkuu wa wizara ya habari mawasiliano na tekmolojia ya Habari selestine Kakele amesema serikali ipo katika hatua za mwisho za kukamilisha mapitio ya maboresho ya sera ya Tehama ili kuweza kuwezesha biashara za kimataifa kufanyika kidijiti
Ameyasema hayo katika maonesho ya sabasaba baada ya kutembelea banda la shirika la mawasiliano nchini TTCL ambapo amebainisha kuwa shirika hilo limepiga hatua katika utoaji na usambazaji wa huduma za mawasiliano ya internet nchini
“kukamilika kwa sera yetu kunazidi kujenga mazingira mazuri ya kuvutia uwekezaji hapa nchini, si tu katika tehama lakini katika sekta nyingine za kijamii na kiuchumi tukizungumzia afya, kilimo na elimu”