Home Kitaifa KUBECHA AINGIA KWA KISHINDO TANGA, ZIARA ZAKE KWENYE TAASISI ZA DINI ZAWAFURAHISHA...

KUBECHA AINGIA KWA KISHINDO TANGA, ZIARA ZAKE KWENYE TAASISI ZA DINI ZAWAFURAHISHA WANATANGA

Ashrack Miraji Tanga

Mkuu wa Wilaya ya Tanga, Mhe. Japhari Kubecha, ameanza ziara zake za kukutana na makundi mbalimbali ya kijamii, zikiwemo taasisi za kidini.

Mhe. Kubecha amehamishiwa Wilaya ya Tanga akitokea wilayani Lushoto, alikokuwa akihudumu kama mkuu wa wilaya hiyo kwa muda wa miezi mitano.

Ni wiki mbili tangu ameripoti na kuanza rasmi majukumu yake katika kituo chake kipya cha kazi.

Tangu ameripoti, ameshafanya ziara kadhaa ikiwemo kutembelea miradi ya maendeleo kama Hospitali ya Wilaya ya Tanga kujionea hali ya utoaji huduma, ametembelea machinjio ya wilaya yaliyopo Mtaa wa Sahare, Kata ya Mnyanjani, ametembelea viwanda kadhaa kujionea ufanisi wake na changamoto zilizosababisha baadhi ya viwanda kutofanya kazi, na makundi ya kijamii wakiwemo wanamichezo, viongozi wa dini na wazee maarufu.

Sasa anaendelea kutembelea taasisi za dini kama Zahran na Shamsul Maarifa leo.

“Nimeanza kufanya ziara kwenye maeneo mbalimbali ndani ya wilaya hii. Lengo langu hasa ni kutaka kujionea mafanikio ya serikali pamoja na changamoto ambazo zinawakabili wananchi na kuweza kuzitatua maana lengo la serikali yetu ni kutatua changamoto kwa wananchi. Pia taasisi za dini ni nguzo muhimu sana kwenye maendeleo ya jamii yetu, hivyo nimeweza kupita huko kuendelea kukutana na viongozi mbalimbali wa dini,” alisema DC Kubecha.

Katika ziara hiyo, DC Kubecha amezitumia kuomba ushirikiano na kusisitiza umoja, mshikamano na maendeleo ya wilaya pamoja na kuelezea mikakati ya kuiongoza Wilaya ya Tanga.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!