Home Kitaifa KONGAMANO LA KUTOKOMEZA MILA POTOFU KUFANYIKA MKOANI TANGA

KONGAMANO LA KUTOKOMEZA MILA POTOFU KUFANYIKA MKOANI TANGA

Na Boniface Gideon, TANGA

Kongamano la kutokomeza maadili potofu kwa hasa  rika la watoto litakalohusisha madhehebu mbalimbali linatatajiwa kufanyika jumamosi hii katika viwanja vya Pongwe jijini Tanga hii ikiwa ni jitihada za kuunga mkono juhudi zinazofanywa na wadau wa  maendeleo ya jamii pamoja na serikali katika kupiga vita vitendo vya ukatili dhidi  kwa  watoto ndani ya  jamii.

Kongamano hilo litaambatana na zoezi la upandaji wa miti katika viunga hivyo ikiwa ni kuhamasisha jamii utunzaji wa mazingira ili kuepukana na athari mbalimbali  ikiwa ni pamoja na mabadiliko ya tabia nchi.

Akizungumza muandaaji wa kongamano hilo ambaye pia ni mchungaji wa  kanisa la Tanzania  Assembly of God ‘TAG’ mtoto wa simba wa kabila la Yuda  na mwalimu wa  mtoto mashuleni Agnes Willium alisema kuwa  kumekuwa masuala ya malezi ya kiimani kana kwamba yametupiliwa mbali jamii  hivyo kupelekea  janga la mmomonyoko wa maadili hasa kwa watoto  wengi kufanyiwa vitendo vya ukatili jambo ambalo linakiuka taratibu na haki za kibinadamu huku viongozi wa dini nao wakihusishwa katika kutekeleza vitendo hivyo.

Alisema ni matarajio makubwa kama jamii inaweza kubadilika ikishirikiana kwa pamoja na juhudi za serikali pamoja na wadau mbalimbali  wa maendeleo huku akielekeza  zaidi kumlea mtoto ambao ni taifa tegemezi la kesho kupitia malezi  kiimani ambayo yatachangia kwa kiasi kikubwa kupungua kwa vitendo vya ukatili.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!