Home Kitaifa SHAKA AMUMWAGIA SIFA KINANA, ATAMBA KAZI ZA MAENDELEO KUUFUTA UPINZANI MBEYA

SHAKA AMUMWAGIA SIFA KINANA, ATAMBA KAZI ZA MAENDELEO KUUFUTA UPINZANI MBEYA

Demokrasia ya vyama vingi nchini imekuwa na lengo la kuharakisha maendeleo kwa wananchi. Ikiwa chama kinachoongoza serikali kinaifanya kazi hiyo kwa weledi wananchi hawana haja ya kujaribu vyama vingine vya kisiasa vilivyopo. Hivyo kwa kazi kubwa na nzuri ya maendeleo inayofanywa mkoani Mbeya na serikali ya CCM inayoongozwa na Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan upinzani utafutika katika mkoa huo.

Hayo yamesemwa na Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Itikadi na Uenezi Ndg Shaka Hamdu Shaka alipokuwa akizungumza katika mkutano wa ndani wa viongozi na wanachama wa chama hicho Jijini Mbeya.

Kwa kazi kubwa inayofanywa na serikali ya CCM chini ya Jemedari Samia Suluhu Hassan siuoni upinzani kuelekea 2024/2025. CCM tunaitekeleza Demokrasia ya kweli kwa vitendo kwa kuhakikisha maendeleo na ustawi wa wananchi yanapatikana. Niwatake wananchi kuendelea kuiamini CCM na serikali yake.” Amesema Shaka

Shaka pia amemmwagia sifa Makamu Mwenyekiti wa chama hicho Tanzania Bara Ndg Abdulrahman Omari Kinana na kusema amekuwa chaguo sahihi kwa nafasi hiyo hivyo kwa niaba ya wanaCCM kote nchini wanamshukuru Mwenyekiti wa chama hicho Ndg Samia Suluhu Hassan kwa kumpendekeza na kuchaguliwa kwa asilimia mia moja na mkutano mkuu wa Taifa.

Komredi Kinana ni gwiji la siasa za ndani na nje, amekulia ndani ya TANU na CCM. Ni mwana majumui (panafricanist). Kwa vijana wenzangu mliyo madarakani na ambao mnatarajia kuingia, Tujifunze kutoka kwa Mzee Kinana, huyu ni chuo kikuu cha siasa kinachotembea, tunaimani naye kuwa atakuwa msaada mkubwa kwa chama chetu.” Alieleza Shaka

Shaka yupo ziarani mkoani Mbeya alipokuwa ameambatana na Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara ambapo wamehitimisha leo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!