Home Kitaifa KIVUKO CHA GONZAGA KUPEWA JINA LA SHIGULA

KIVUKO CHA GONZAGA KUPEWA JINA LA SHIGULA

Waziri wa Nchi OR-MU na Mbunge wa Jimbo la Ubungo Prof. Kitila Mkumbo akiwa ziarani katika Kata ya Mabibo amejadiliana na kukubaliana na Viongozi wa Kata hiyo kutoa jina la Shigula kwa kivuko cha Gonzaga kutokana na chimbuko la kivuko hicho.

Uamuzi huo umefikiwa kufuatia siku ya msiba wa aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM Kata ya Mabibo mwaka mmoja uliopita
Edward Shigula Viongozi wa Kata ya Mabibo waliomba kujengwa kwa kivuko hicho kinachowaunganisha wakazi wa Mabibo na Kigogo jambo ambalo lilifanyika.

Akiwa ziarani Mabibo Prof. Kitila Mkumbo amesema ni heshima kumuenzi Kiongozi huyo badala ya kutumia majina ya Viongozi wengine kwenye kivuko hicho ambacho ujenzi wake ulitokana na msiba wa Shigula baada ya Viongozi wengine kuomba.

Tunatakiwa kuwa na utaratibu wa kuwaenzi Viongozi waliopo kwenye maeneo yetu, siyo kila kitu kinapewa jina la Kiongozi mkubwa ambaye hata hajahusika katika kwenye jambo lenyewe, hapa tukiita kivuko cha kumbukumbu ya Shigula itakaa vizuri” Prof. Kitila Mkumbo.

Baada ya makubaliano hayo Prof. Kitila amewaagiza Viongozi wa Kata ya Mabibo kupata ridhaa ya familia ya Edward Shigula kabla ya kutumia jina hilo.

=======

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!