Home Michezo KITAJI FC WAIPA KICHAPO CHA 4-0 IRINGO FC MASHINDANO YA MATHAYO CUP

KITAJI FC WAIPA KICHAPO CHA 4-0 IRINGO FC MASHINDANO YA MATHAYO CUP

Na Shomari Binda-Musoma

TIMU ya Kitaji fc imeanza vyena mashindano ya Mathayo Cup baada ya kuipa kichapo cha bao 4-0 timu ya Iringo fc.

Hadi kipindi cha kwanza kinamalizika tayari vijana wa Kitaji fc walikuwa mbele kwa bao 2-0 huku Iringo fc wakionekana kuzidiwa kila eneo.

Kipindi cha pili timu zote zilianza kwa kasi ya kutafuta mabao lakini bahati ilikuwa upande wa Kitaji fc walioongeza mabao mengine mawili na kufikisha 4 hadi dakika 90 zinamalizika.

Akizungumza mara baada ya mchezo huo kumalizika,kocha wa timu ya Kitaji fc,Zamoyoni Taruma, amesema wachezaji wake wamecheza vizuri na ndio kilichowapa matokeo.

Amesema mwanzoni wapinzani wao walionekana kutoa ushindani na kubadili mfumo uliowapa matokeo.

Diwani wa Kata ya Iringo timu yake iliyopoteza mchezo,Juma Hamisi(Igwe) amesema wamepoteza mchezo dhidi ya Kitaji kutokana na kucheza vibaya na kudai benchi la ufundi linakwenda kufanyia kazi makosa.

Katika mchezo uliochezwa mapema kwenye uwanja huo wa Posta,timu ya Mwigobero fc imetoshana nguvu na Mukendo fc kwa kufungana bao 2-2

Kesho jumanne mashindano hayo yataendelea tena kwenye uwanja wa Buhare chuoni ambapo kwenye mchezo wa mapema sàa 8 timu ya Makoko fc itaikaribisha timu ya Mwisenge fc huku majira ya saa 10 jioni Buhare fc itawaalika Kamnyonge fc.

Bingwa wa mashindano haya yatakayodumu kwa mwezi mmoja yaliyoandaliwa na mbunge wa jimbo la Musoma mjini,Vedastus Mathayo,ataondoka na zawadi ya ng’ombe huku mshindi wa pili akiondoka na shilingi laki 5 na mbuzi mmoja.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!