Na Magrethy Katengu
Jeshi la Polisi limetakiwa kwenda kidigitali kwani Dunia sasa ipo kiganjani ili kusaidia kudhibiti uhalifu kwani uhalifu umekuwa ukitendeka katika mitando ikiweno wizi wa fedha , usafirishaji dawa za Kulevya kwa njia ya mtandao, .
Agizo hilo limetolewa Jijini Dar es salaam na Naibu Waziri Jumanne Sagin Wakati wa hafla ya Uzinduzi wa kitabu cha Polisi “Utawala na Usimamizi wa Sheria Tanzania “kilichobeba ujumbe Mkakati wa kubadili Mwelekeo kilichoandikwa na Mkuu wa Zamani Jeshi la Polisi (IGP) Saidi Ally Mwema aliongoza Jeshi mwaka 2006-2013 ambapo amesema sasa ni ukweli ulio wazi kwamba teknolojia inapaswa kuwa msingi wa maendeleo ya polisi katika majukumu yao ya kudhibiti uhalifu ili kusaidia usalama wa raia na mali zao .
“Nimesoma kitabu hiki kwa makini sana nimeona tunu kubwa tuliachiwa kama Taifa na IGP wetu Mstaafu ameweka nukuu kadhaa za ujuzi maarifa yake na ameonesha aina mpaya ya Mwelekeo Jeshi livyotakiwa kutumia TEHAMA ili kusaidia kudhibiti uhalifu kwani Dunia ipo kiganjani huvyo Jeshi someni kitabu hiki ili mpate nasaha zitakazowasaidia” amesema Naibu Waziri
Hata hivyo amesema Jeshi linatakiwa kuwa la kisasa zaidi katika kuhakikisha Sheria zinafuatwa kutokana na kuwa msongamano wa maisha ya kidigitali kuathirika kwa matumizi mabaya ya kidigitali hivyo lazima mifumo ya kiteknolojia ya Jeshi iimarishwe zaidi
Naye Kamishna Mstaafu wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Dar es Salaam Kamanda Kova amempongeza IGP Mstaafu kuzindua kitabu chake kwani kitakuwa msaada na Jeshi linamkumbuka kwa Kwa mambo mengi aliyoyafanya na ameandika kitabu hicho kwa nakala ya lungha ya Kiswahili na Kingereza kila mmoja asome apate maarifa.
“Nitoe ushuhuda wangu Mimi Kova wakati nateuliwa kwenda Mbeya kwenda kuwa Mkuu wa Jeshi la. Polisi na Wakati ule Mbeya matukio yaliyosheheni ni mauji uchunaji ngozi nilikuwa wa kwanza kutoa namba za simu kwa wananchi ili nipate taarifa na nilifanikiwa kukomesha uhalifu ulioingia na kweli ninakiri teknolojia inasaidia sanaa” amesema Kamishna Mstaafu Kova..
Naye IGP Mstaafu Saidi Mwema ameshukuru wote waliokuwa naye katika uongozi wake na wale wote waliofanikisha kuandika kitabu chale ikiwemo Rais Mstaafu Jakaya Kikwete ameandika naye nukuu ili kusaidia kila mmoja asome na aelewe.
“Nilizaliwa miongoni mwa Watanzania nikakua miongoni mwa watanzania na kusomeshwa na watanzania nikapewa fursa ya ya maarifa na uzoefu hivyo nami nimeandika mambo mengi kwa watanzania,kitabu hiki nakitoa kwa watanzania na kitasambazwa bure Nchi nzima kwani maandalizi yake yamefadhiliwa na wadau” amesema IGP Mstaafu Mwema
Aidha uzinduzi huo ulihudhuriwa na Wageni mbalimbali ndani na Nje ya nchi ikiwemo Mwakilishi wa Ubalozi wa Ujeruma, Othman Chande Jaji Mkuu mstaafu na Mwenyekiti wa Tume ya Haki Jinai.
Katibu Kiongozi mstaafu Ombeni Sefue,Mkuu wa Jeshi la Polisi mstaafu IGP Ernest Jumbe Mangu na wajumbe wengine toka Tume ya Haki Jinai na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Hanns Seidel Foundation Mhe.Karl-Peter Schöndorfich,Rais mstaafu wa Jeshi la Polisi jimbo la Bavaria Wolfgang na Maafisa wa Polisi kutika Royal Thai Police Thailand, Kamishna wa Polisi Zanzibar CP Hamad Khamis Hamad,Kamishna wa Utawala na Menejimenti ya raslimali watu CP Suzan Kaganda
Pia waliofanya uchambuzi (penalists) wa kitabu hicho mbele ya wageni ni Dr. Hildebrand Shayo,Prof.Semboja na Kamishna wa Polisi Suzan Kaganda.