Home Kitaifa KINANA:VIONGOZI SERIKALINI FUATENI NYAYO ZA RAIS SAMIA KUESHIMU SHERIA, KANUNI MNAPOCHUKUA HATUA...

KINANA:VIONGOZI SERIKALINI FUATENI NYAYO ZA RAIS SAMIA KUESHIMU SHERIA, KANUNI MNAPOCHUKUA HATUA DHIDI YA WATENDAJI

Na Mwandishi Wetu

MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, Abdulrahman Kinana ametaka viongozi na watenaji serikalini kuzingatia kanuni, sheria, utaratibu na Katiba wanapowakosoa watendaji.

Amesema ni vyema wakajifunza kwa Rais Dk. Samia Suluhu Hassan ambaye pamoja na kuwa na uwezo na mamaka lakini hajawahi kusimama hadharani na kuvunja haki ya utu wa mtu hususan watendaji katika ngazi mbalimbali.

Kinana aliyasema hayo jana Ushirombo, Wilaya ya Bukombe mkoani Geita alipokuwa akizungumza na wanachama wa CCM, viongozi na wananchi alipofungua jengo la ofisi za CCM la wlaya hiyo.

Nataka kufafanua hili ambalo nimezungumza katika Mkutano Mkuu hapa Bukombe, ni kwamba viongozi wasimamie watendaji serikalini, wasimamie sheria, kanuni na utaratibu lakini si vizuri kuwasema hadharani na kuwafedhehesha watendaji wa serikali.

Mfano mzuri wa kuigwa ni wa Rais Dk. Samia Suluhu Hassan kwani hatujawahi kuona akisimama hadharani akmfedhehesha mtendaji serikalini, kwa sababu yeye ni muumini wa utawala bora, unaozingatia katiba, sheria, kanuni na taratibu,” alisema.

Kinana alsisitiza watendaji wote wa serikali wanasimamiwa na kanuni, sheria, katiba na utendaji serikalini.

Pia, alieleza kuwa watendaji hao wanasimamiwa na tume mbalimbali zinazosimamia maadili ya utendaji pamoja na nidhamu serikalini, hivyo ni vizuri kutumia utaratibu huo.

Ninyi wenyewe mmeona mfano mzuri wa Rais, tuige huu mfano, Rais hajawaji kusimama hadharani hata siku moja akamfukuza mtumishi kazi kwa kuwa anaelewa utararibu na amekuwa akizingatia utaratibu huo, tunawataka viongozi na watendaji serikalini kuzingatia utararibu hizo.

Mfano mwingine naweza nikawapa kuna ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), kwa kuzingatia ripoti ya CAG Rais anauwezo wa kumfukuza mtu yeyote wakati wowote kwa sababu anazozijua yeye,” alieleza.

Kwa mujibu wa Kinana, Rais Samia hafanyi hivyo bali husubiri utaratibu na kanuni zifuatwe kwa sababu anaweza kumfukuza au kumsema mtu hadharani lakini baadaye ikabainika hana kosa “sasa unamuombaje radhi.”

Aliwataka viongozi kuurudisha utaratibu wa kuzingatia utawala bora, kuheshimu sheria, kwani hata Katiba inasema kwamba utu wa mtu ni lazima uheshimiwe na kwamba kwa kuzingatia hilo Rais Dk. Samia anaonesha mfano kwa vitendo.

Aidha alimpongeza Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Dkt. Doto Biteko (Mbunge wa Bukombe)  kwa kubuni na kuleta mawazo hayo ya ujenzi ambayo yalienda Kamati ya Siasa na Halmashauri Kuu na baadaye Wanachama na hivyo  uamuzi wa kujenga majengo hayo ulifanyika.

Kutokana na ujenzi wa majengo ya CCM, Bukombe kumfurahisha Komredi Kinana,  ameitaka CCM, Mkoa wa Dar es Salaam kujenga Ofisi za kisasa za CCM katika Wilaya zake kama ilivyo Bukombe.

Alisema  WanaCCM nchi nzima wana wajibu wa kuhakikisha kuwa, Ofisi wanazojenga na kumbi zinafanana na heshima na hadhi ya ukubwa wa CCM kama ambavyo Bukombe walivyotoa heshima hiyo kwa Chama cha Mapinduzi.

Aidha, Kinana amepongeza umoja na mshikamano ulioko wilayani Bukombe pamoja na Mkoa wa Geita kwa ujumla na kueleza kuwa wao ni Walimu wazuri wa Kusema na Kutenda hivyo atawatuma viongozi wa Chama wa Mikoa na Wilaya  kutoka maeneo mbalimbali nchini, waende Bukombe kujifunza mfano wa kuimarisha Chama Kitaasisi na kujitegemea.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!