Home Kitaifa KINANA AZIHIMIZA TAASISI ZA KIJAMII KUJIKITA KATIKA UFUNDI, UJASIRIAMALI.

KINANA AZIHIMIZA TAASISI ZA KIJAMII KUJIKITA KATIKA UFUNDI, UJASIRIAMALI.

MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, Abdulrahman Kinana, amezihimiza taasisi za kijamii kuweka mkazo katika elimu ya ufundi na ujasiriamali, ili kupata mwarobaini wa tatizo la ajira na kuzalisha wataalamu wengi zaidi wa fani mbalimbali.

Kinana ameyasema hayo leo, Desemba 24, 2023, jijini Arusha, alipokuwa mgeni rasmi katika Mkutano Mkuu wa 10 wa Jukwa la Vijana wa Kiislamu Mkoa wa Arusha (JUVIKIBA).

Kinana amesema kuwa, endapo taasisi za kijamii zitajikita kuhamasisha elimu ya amali (ufundi), vijana wengi watapata utaalamu katika fani mbalimbali ambao utawawezesha kujiajiri, kuajiri wenzao na hata kuwa na sifa ya kuajiriwa katika maeneo mbalimbali ya fani walizozisomea na kujifunza.

Aidha, amewapongeza vijana wa jukwaa hilo kwa kujitoa kupambania elimu ya ujasiriamali na ufundi ambapo amesisitiza kuwa anaamini jitihada hizo zitawalipa matunda mema kwa kujiingizia kipato badala ya kusubiri ajira kutoka serikalini.

Pia Ndg Kinana Ameipongeza benki ya KCB kwa kufadhili Maadhimisho ya miaka kumi ya Jukwaa hilo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!