Home Kitaifa KINANA ASIFU UZALENDO, UTAIFA WA NYERERE, JENERALI MUSUGURI.

KINANA ASIFU UZALENDO, UTAIFA WA NYERERE, JENERALI MUSUGURI.

MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara Kanali Mstaafu Abdulrahman Kinana amezulu kaburi la hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere na kueleza kuwa ni mwanamapinduzi wa kweli na shujaa wa Afrika.

Amesema wakati Tanzania ikiadhimisha siku ya mashujaa, Mwalimu Nyerere anabaki kuwa shujaa namba moja wa Tanzania huku pia akimtembelea Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi mstaafu Jenerali David Musuguli (103) na kumwelelezea ni alama ya uzalendo wa Taifa, ni alama ya ukombozi na anastahili kuombewa afya njema.

Kanali Mstaafu Kinana ameyasema hayo leo Julai 25, 2023 baada ya kuzulu kaburi la Mwalimu Nyerere na kumtembelea Mzee Musuguli nyumbani kwake Butiama mkoani Mara akiwa katika ziara kukagua uhai wa Chama, utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM na kuzungumza na wanachama.

Akiwa katika kaburi la Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere na baada ya kuweka shada la maua, Kinana amemwelezea kuwa ni shujaa wa Tanzania na Afrika na kutoa mwito kwa nchi zinazotamani kuzikalia nchi nyingine kiuchumi kuiga mema ya baba wa Taifa ambaye aliongongoza mapambano ya kumaliza udhalimu wa nduli Idd Amin nchini Uganda.

Aidha, akiwa nyumbani kwa Jenerali Musuguri, Kinana alimwelezea kuwa mzalendo wa kweli aliyeongoza mapambano dhidi ya Idd Amin.

Jenerali Musuguli ameliongoza Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania kwa zaidi ya miaka 50, ameliongoza Jeshi katika nafasi mbalimbali, wakati leo tunaadhimisha miaka 44 ya vita ya Uganda Jenerali Musuguli ndiye aliyeyaongoza majeshi ya Tanzania kumng’oa Nduli Idd Amin,” amesema.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!