Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi Vijana Ajira na Wenye Ulemavu Ridhiwani Kikwete awapongeza timu ya Simba kwa kuingia hatua ya makundi na kusema kuingia kwao kwenye hatua hiyo ni ushindi mkubwa kwa taifa.
Amesema hayo katika hafla fupi ya kupokea msaada kutoka Banki ya NMB wa vitanda vitano, mashuka 100 ya Hospitali ya wilaya ya Msoga na madawati 150 ya Shule za msingi mbili za Jimbo la Chalinze, hafla iliyofanyika katika hospitali ya Msoga Wilayani Bagamoyo Mkoani Pwani.
Ridhiwani amesema kwa kuwa michezo ndio inayoipa Heshima nchi yetu ya Tanzania hivyo timu hiyo inastagili kupongezwa.
Aidha Mheshimiwa Ridhiwani amesema mshukuru Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kutoa zaidi ya shillingi Bililoni 5 kwaajili ya kuendeleza ujenzi wa majengo ya Hospitali hiyo inayohudumia pia na wagonjwa kutoka wilaya na mikoa jirani.
Amesema hadi sasa majengo 17 kati ya 22 yamekamilika huku amewataka NMB kuto wachoka kwani hospital hiyo badohaijakamilika ika kwa sasa majengo taliyokamilika ni jengo la dharura, kuhifadhia maiti, jengo la kufulia lenye mashine za kisasa, jengo la.mionzi, na jengo la upasuaji ambapo zaidi ya Bil.5 zimetumika huku ametoa shukrani zake za dhati kwa Mhe.Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwakuwajaliwananchi wa Chalinze.
Donatus Richard – Mkuu wa idara ya Mauzo na Mtandao wa matawi wa Benki ya NMB amesema kuwa kipaumbele cha benki yao ni kusaidia wananchi katika maeneo ya Afya, Elimu na Majanga ikiwa ni kutokana na huduma ya Banki hiyo kutenga asilimia moja ya mapato yake kwa kuhudumia Wananchi.
Hafla hiyo imehudhuriwa na Viongozi mbalimbali wa Chama na serikali ikiwa ni pamoja na Mkuu wa Wilaya mpya Shaibu Ndemanga na Mwenyekiti wa Halmshauri ya Chalinze Hassan Mwinyikondo.