Home Kitaifa KIKONGWE AUAWA NA MJUKUU WAKE MOROGORO

KIKONGWE AUAWA NA MJUKUU WAKE MOROGORO

Jeshi la Polisi mkoani Morogoro linamshikilia Waaki Athumani mkazi wa Mzumbe wilayani Mvomero mwenye umri wa miaka 28 kwa tuhuma za kumuua bibi yake na kitu chenye ncha kali

Akizungumzia tukio hilo Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Morogoro Alex Mkama amesema kuwa tukio hilo limetokea Aprili 6 majira ya saa nane mchana ambapo kijana huyo alimshambulia bibi yake Agness Kalori 70 kwa kutumia panga.

Kwa upande wao ndugu na majirani wamesema kuwa kijana huyo alikuwa na changamoto ya afya ya akili.

“Ndugu yetu anachangamoto ya afya ya akili kwani alianza kuchoma moto nguo zake na baadae akaanza kuchoma moto magodoro na hii ilianza kumtokea wakati akiishi Dar-es-salaam ndio tukafanya jitihada za kumrudisha na kuanza kumtibia na jana ndio akafanya tukio hilo la kumuua Bibi na hili tukio si mara ya kwanza kutokea katika ukoo wetu kwani hata mjomba aliishawahi kufanya tukio kama hili “

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!