Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb.) amechaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Mawaziri wa Eneo Huru la Biashara Afrika (AfCFTA Council of Ministers) kwa kipindi cha mwaka mmoja (1) kuanzia Desemba 07, 2023.
Aidha, Waziri Kijaji ameongoza Mkutano wa 12 wa Baraza la Mawaziri wa Eneo Huru la Biashara Afrika Desemba 7, 2023 ulioanza Desemba 06, 2023 sambamba na Kongamano la Pili la AfCFTA la Wanawake katika Biashara lililoanza tarehe 06 Desemba 2023 katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Mwalimu Julius Nyerere (JNICC) jijini Dar es Salaam.
Mkutano huo chini ya Uenyekiti wa Waziri Kijaji umepitisha Itifaki ya AfCFTA ya Wanawake na Vijana katika Biashara ambayo imekamilika chini ya usimamizi wa Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri na Muungano wa Tanzania na Mhamasishaji Mkuu na Kinara wa Wanawake na Vijana katika Biashara Barani Afrika.