Home Kitaifa KIGERA FC,MWIGOERO FC,MARA SPORTS NA MSHIKAMANO FC ZAFUZU NUSU FAINALI POLISI JAMII...

KIGERA FC,MWIGOERO FC,MARA SPORTS NA MSHIKAMANO FC ZAFUZU NUSU FAINALI POLISI JAMII CUP 2024 MUSOMA

Na Shomari Binda-Musoma

TIMU 4 za Kigera rc,Mwigobero fc,Mara Sports na Mshikamano fc zimefuzu hatua ya nusu fainali ya mashindano ya Polisi Jamii Cup 2024 Wilaya ya Musoma.

Hatua ya makundi ya mashindano hayo imeitimishwa leo septemba 23 kwenye uwanja wa Mara sekondari kwa mchezo kati ya Nyamatare na Ajax fc uliomalizika kwa timu ya

Mchezo wa nusu fainali ya kwanza utachezwa septemba 25 kati ya Kigera na Mshikamano huku nusu fainali ya pili ikichezwa septemba 26 kwa mchezo kati ya Mwigobero fc na Mara Sports

Mmoja wa wasimamizi wa mashindano hayo Omary Girbert amesema haikuwa jambo rahisi kufika hatua hiyo kutokana na ushindani uliokuwepo.

Amesema timu zote 20 zulizishiriki mashindano hayo zilikuwa zimejiandaa vizuri na kulikuwa hakuna timu iliuoyegemewa kuingia hatua hiyo.

Omary amesema anategemea ushindani mkubwa kwenye michezo ya hatua ya nusu fainali kutokana na ugumu wa timu zote.

Amesema timu ambazo zitajiandaa vizuri ndizo zitakazocheza fainali ambayo inatarajiwa kuchezwa septemba 30 kwenye uwanja huo wa Mara sekondari.

” Tunashukuru kufikia hatua hii ya nusu fainali ushindani ulikuwa mkubwa lakini timu hizi 4 zimefanikiwa kuingia nusu fainali.

” Tunategemea ushindani mkubwa kuonekana pia kwenye hatua ya nusu fainali na hadi sasa haitabiriki timu itwkayochukua ubingwa wa mashindano ya mwaka huu”,amesema Omary.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!