Home Kitaifa KIGAHE AZINDUA BARAZA LA SHIRIKA LA VIWANDA LA UTAFITI NA MAENDELEO YA...

KIGAHE AZINDUA BARAZA LA SHIRIKA LA VIWANDA LA UTAFITI NA MAENDELEO YA VIWANDA TANZANIA

NAIBU Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara Exaud Kigahe amezindua Baraza la Shirika la Utafiti wa na Maendeleo ya Viwanda Tanzania (TIRDO).

Akizungumza katika hafla fupi ya uzinduzi wa Baraza hilo uliofanyika leo Septemba 28, 2022 jijini Dar es Salaam, Kigahe amesema Baraza lina jukumu kubwa la kuandaa mkakati wa kuhakikisha kwamba malengo ya Taifa, Wizara na Shirika yanafanikiwa kwa kusimamia utekelezaji wa mipango ya Shirika.

Vilevile, ifahamike kuwa katika hili, Baraza na Menejimenti mtapimwa kwa kutumia mkataba wa utendajikazi (Perfomance Contract) ambao mtausaini Wajumbe wa Baraza kupitia kwa Mwenyekiti wenu na Msajili wa Hazina,” amesema Kigahe.

Naibu Waziri Kigahe amelitaka Baraza hilo kutoa ushauri na unasihi ndani na nje ya vikao vya Baraza, kwamba ushauri aliolenga ni katika maeneo mengi yenye tija kwa shirika kama vile namna ya kutatua changamoto za shirika, mawazo mapya ya kuboresha uendeshaji wa shirika, huduma mpya ambazo shirika linaweza kuzianzisha katika kuimarisha utendaji wake na kutatua migogoro ambayo inaweza kujitokeza wakati wa utekelezaji wa majukumu.

Hivyo amesema ili wajumbe wote waweze kulifanya jukumu hilo kwa weledi ni lazima wawe na uelewa mpana kuhusu TIRDO, wadau muhimu wa Shirika na mwelekeo wa kisera wa nchi.

Kigahe ameeleza kwamba Baraza linatarajiwa kuwa mtunza nidhamu wa Menejimenti na watumishi wa Shirika hilo kwa niaba ya Serikali, kwamba jukumu hilo ni kimsingi linawapa uhalali wa kuhakikisha kuwa Menejimenti inatekeleza majukumu yake kwa ufanisi na kwa kufuata Sheria, Kanuni na Taratibu za nchi.

Ameipongeza Menejimenti ya TIRDO kwa kusimamia vizuri utekelezaji wa majukumu ya Shirika kipindi chote ambacho Shirika lilijiendesha pasipokuwa na Baraza.

Nimeona vile vile, bunifu mbalimbali ambazo zimelenga kuleta suluhisho kwa Watanzania kwa kusaidia teknolojia rahisi za kuongeza thamani ya mazao na hivyo kuwezesha uanzishwaji wa viwanda vidogo na vya kati,” ameongeza Kigahe.

Hivyo ametoa rai kwa Baraza na Mejimenti, kuendelea kuandika maandiko mbalimbali (project proposals) kwenda kwa wadau mbalimbali wa kisekta ili waweze kupata fedha za utafiti na hatimaye kubuni teknolojia ambazo zitaendelea kuwasaidia wakulima, wavuvi na sekta zingine zote na ajira kupitia viwanda vitakavyoanzishwa.

Aidha ametaka teknolojia watakazobuni ziwe za bei rahisi kulingana na uwezo wa wakulima, wafugaji na wajasiriamali.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!