Home Kitaifa KIBAHA WAFANYA KUMBUKIZI YA MIAKA 24 YA KIFO CHA BABA WA TAIFA...

KIBAHA WAFANYA KUMBUKIZI YA MIAKA 24 YA KIFO CHA BABA WA TAIFA MWALIMU JULIUS KAMBARAGE NYERERE KWA KUFANYA HARAMBEE YA KUMALIZIA UJENZI WA SHULE YA MSINGI KAMBARAGE

Na Scolastica Msewa
Zaidi ya Shilingi milioni 14. 7 na mifuko ya 880 ya saruji imepatikana katika harambee ya kukamilisha vyumba vitano vya madarasa na vyoo 26 katika Shule ya msingi Kambarage ikiwa ni Maadhimisho ya miaka 24 ya Kumbukumbu ya kifo cha Baba wa Taifa Mwalimu julias Kambarage Nyerere kiwilaya Wilayani Kibaha mkoani Pwani.

Harambee hiyo iliyofanyika kwa ushiriano Taasisi ya kumbukumbu ya Mwalimu Julias Nyerere mkoa wa Pwani na Uongozi wa Mkuu wa Wilaya ya Kibaha Nickson John, Ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Kibaha Eng. Mshamu Munde ambapo Mgeni rasmi katika Maadhimisho hayo alikuwa Kaimu Meneja wa MFUKO WA TAIFA WA Hifadhi ya Jamii NSSF mkoa wa Pwani Heri Abdi Kasingo.

Ambapo mbali ya kiasi hicho cha fedha kilichopatikana pia ilipatikana Dola za kimarekani 58, ahadi ya Madawati 50, nondo 62 na mchanga malori mawili.

Hatahivyo Chama Cha Mapinduzi kupitia Mwenyekiti wa jumuhiya ya Wazazi mkoa John Kituka aliongoza viongozi mbalimbali wa CCM ambapo zaidi ya shilingi milioni 2 ziliahidiwa na mifuko zaidi ya 300 ya saruji.

Katibu wa Taasisi ya kumbukumbu ya Mwalimu Julias Nyerere mkoa wa Pwani Omari Punzi alisema majukumu ya taasisi hiyo ni kushirikiana na serikali katika kutafutia ufumbuzi kero na changamoto mbalimbali zilizopo katika jamii Kama hiyo ya kushughulikia upungufu wa vyumba vya madarasa na vyoo kwaajili ya wanafunzi wa Shule ya msingi Kambarage.

Omari amesema taasisi hiyo ya kumbukumbu ya Mwalimu Julias Nyerere mwaka huu imeungana na Watanzania wote kukumbuka kifo cha Muasisi na Baba wa Taifa kwa kukusanya Wadau mbalimbali wa Maendeleo wa mji wa Kibaha ambao wamechangishana fedha na vifaa hivyo vya ujenzi ili kufanikisha upatikanaji wa jawabu la mahitaji ya shule hiyo ya msingi Kambarage.

Mkuu wa Wilaya ya Kibaha Nickson John amesema lengo la kufanya harambee hiyo ni kupata fedha ambazo zitasaidia kukamilisha vyumba hivyo vya madarasa na vyoo 26 ili hadi kufikia mwakani viwe vimekamilika.

Aidha Akizungumzia mahitaji ya vyumba vya madarasa Wilaya nzima ya Kibaha amesema anashukuru uongozi wa serikali ya awamu ya sita kwa jitihada kubwa za kujenga vyumba vya madarasa ambapo zaidi ya asilimia 90 ya mahitaji yamefanikishwa.

Kaimu Meneja wa MFUKO WA TAIFA WA Hifadhi ya Jamii NSSF mkoa wa Pwani Heri Abdi Kasingo amepongeza jitihada kubwa zilizofanywa na Uongozi wa Shule na Uongozi wa Wilaya ya Kibaha alitoa ahadi ya shilingi milioni 2 kwaajili ya kukamilisha ujenzi huo.

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Kibaha Eng. Mshamu Munde amesema bajeti ya fedha ya Halmashauri hiyo ya mwaka wa fedha wa 2024/2025 upande wa elimu itajikita kumalizia maboma ya Shule za msingi na Sekondari kwa lengo kumaliza kero ya upungufu wa vyumba vya madarasa Wilaya humo.

Diwani wa Kata ya Tumbi Raymond Chokala ameshukuru kwa michango mbalimbali ya hali na mali ilikufanikisha ujenzi huo sambamba na kuwaalika Wadau mbalimbali wa Maendeleo kuendelea kuchangia miradi ya maendeleo katika Kata hiyo.

Naye Mwalimu Mkuu wa Shule ya msingi Kambarage Happiness Msaki amesema kupitia harambee hiyo wamepunguza upungufu mkubwa wa vyumba vya madarasa na kuahidi kuongeza ufaulu kwa wanafunzi watakaomaliza darasa la saba mwakani.
++++++++

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!