Home Kitaifa KIBAHA: BARAZA LA MADIWANI LAAGIZA KUWAUA MBWA WASIO NA WALEZI

KIBAHA: BARAZA LA MADIWANI LAAGIZA KUWAUA MBWA WASIO NA WALEZI

BARAZA la Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha wameiagiza Halmashauri hiyo kuwaua mbwa ambao hawana walezi kuepuka madhara ambayo yanaweza kutolea.

Wamefikia hatua hiyo baada ya kuwepo kwa taarifa za idadi kubwa ya mbwa ambao hawajapata chanjo na wanaendelea kuzurura mitaani huku kila mwananchi akikwepa kuwa mmiliki wa mbwa hao.

Akizungumza katika kikao Baraza la Madiwani kilichofanyika Mjini Mlandizi ambapo Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Erasto Makala alisema mbwa ambao hawana walezi wanatakiwa kuuwawa kama tahadhari ya madhara ambayo yanaweza kutolea.

Awali akiwasilisha hoja kuhusiana na mbwa hao katika kikao hicho Diwani Shomari Mwinishehe amesema taarifa ya idara ya mifugo imebainisha kuwatambua mbwa 4,338 hadi sasa waliopata chanjo ni mbwa 312 Hali ambayo inaonyesha kuwepo kwa kasi ndogo ya uchanjaji wa mbwa hao.

Tunaelezwa chanjo iliyoagizwa ni 628 sasa Hawa mbwa wengine zaidi ya 3000 wakiachwa bila kuchanjwa hapo madhara ambayo yatatokea kwa Jamii mbaya zaidi kila ukiuliza mlezi wa mbwa hao mtaani kila mtu anawakataa,” ameeleza Shomari.

Kutokana na Hali hiyo Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha Regina Bieda ameahidi kufanyia kazi agizo hilo kuepusha madhara kwa Jamii.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!