Home Kitaifa KHERI JAMES: AMELIPONGEZA KANISA KATOLIKI JIMBO LA MBULU KWA MCHANGO WAKE KATIKA...

KHERI JAMES: AMELIPONGEZA KANISA KATOLIKI JIMBO LA MBULU KWA MCHANGO WAKE KATIKA MAENDELEO

Mbulu-Manyara.

Mkuu wa wilaya ya Mbulu Komred Kheri James,amelipongeza kanisa Katoliki Jimbo la Mbulu kwa mchango wake mkubwa katika Harakati za Maendeleo na Usimamizi wa Malezi na Maadili katika Jamii ya Mbulu.

Komred Kheri James ameyasema hayo hii Leo Februari 21, 2023 katika adhimisho la Misa Takatifu ya kumshukuru Mungu kwa miaka 25 ya ukasisi wa Padre Emanuel Geay wa Parokia ya Karatu Mjini, ilio fanyika katika Parokia ya Sanu wilayani Mbulu.

Katika hotuba yake Komred Kheri James amepongeza Kazi Kubwa na Nzuri inayo fanywa na Kanisa Katoliki jimbo la Mbulu chini ya Uongozi wa Mhasham Baba Askofu Antony Lagwen, na ameeleza kuwa kazi hiyo imesaidia sana katika Kuchochea Harakati za Maendeleo, kuimarisha Umoja na Kujenga Msingi wa Malezi na Maadili Mema katika Jamii ya wana Mbulu.

Kupitia Adhimisho hilo la Misa Takatifu, Komred Kheri James amewakikishia viongozi na Taasisi za kidini wilayani Mbulu kuwa, Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Uongozi wa Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, itaendelea Kutoa Ushirikiano wa dhati kwa Viongozi na Taasisi zote za Dini chini katika kutimiza Malengo waliojiwekea Pamoja na Kutumia Vyema Haki na Uhuru wao wa kufanya ibada.


Adhimisho hilo la Misa Takatifu limehudhuriwa na Viongozi wa klkanisa Katoliki wakiongozwa na Mhasham Baba askofu wa Jimbo la Mbulu, Waheshimiwa Wabunge wa wilaya ya Mbulu, Viongozi wa Taasisi na Jumuiya mbalimbali, Pamoja na Waamini na Wananchi.

Kwapamoja,tunaijenga Mbulu yetu.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!