Home Biashara KERO YA USHURU SOKO LA MCHELE LA MAGUGU KUFANYIWA KAZI

KERO YA USHURU SOKO LA MCHELE LA MAGUGU KUFANYIWA KAZI

Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara Dkt. Ashatu Kijaji (Mb.) amewaahidi wafanyabiashara wa soko la mchele la Magugu mkoani Manyara kufanyia kazi kero ya utozaji wa ushuru wa Shilingi 1500 kwa mfuko wa ujazo wa kilo 50 na kwa kushirikiana na Waziri wa Kilimo pamoja na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tamisemi.

Waziri Kijaji ametoa ahadi hiyo Mei 12, 2023 alipotembelea soko la mchele la Magugu mkoani Manyara
na kukutana na Wafanyabiashara kwa lengo la kujionea hali ya biashara katika soko hilo wakati wa mwanzo wa msimu wa mavuno ya Mpunga kwa mwaka 2023.

Wakiongea na Waziri Kijaji, Wafanyabiashara wa Magugu wameipongeza Serikali kwa kusaidia kuboresha mazingira ya Wafabyabiashara wadogo na wameiomba Serikali iwapunguzie tozo ya ushuru wa Shilingi 1500 kwa mfuko wa ujazo wa kilo 50 kwa kuwa inaongeza gharama katika biashara.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!