Na Shomari Binda-Musoma
KAZI zinazofanywa na madiwani wa viti maalum manispaa ya Musoma zimepokelewa na kupongezwa na wajumbe wa Baraza la UWT Wilaya ya Musoma mjini.
Wakizungumza mara baada ya madiwani 5 kuwasilisha taarifa zao za kazi kuanzia januari 2023 hadi disemba 2024 wamesema wanaridhishwa na kazi zao
Wajumbe hao ambao ni Mwenyekiti na Katibu kutoka Kata 16 za manispaa ya Musoma wamesema kilichowasilishwa na madiwani hao wameyakubali maana yalifanyika kwenye Kata zao
Wamesema uhamasishaji wa vikundi waliufanya na vikundi kuanzishwa na vingine tayari vimeshapata mikopo ya asilimia 10 inayotolewa na halmashauri ya manispaa ya Musoma.
Kwa kauli moja wajumbe hao wamesema wanapokea kazi walizofanya kwa mikono miwili na wametekeleza majukumu yao.
” Mwenyekiti tumepokea taarifa za madiwani wetu na tunazipokea kwa mikono miwili maana kazi walizozifanya tumeziona na tumewaona kwenye Kata zetu”,wamesema.
Mwenyekiti wa UWT Wilaya ya Musoma Stera Mtani amewapongeza madiwani hao kwa kazi walizofanya na kupokelewa na kikao cha baraza
Amesema kama Mwenyekiti wao amefurahi kuona wajumbe wamepokea taarifa ya kazi zao wanazozifanya kwa wananchi.
Madiwani hao kwa nyakati tofauti wamesema walichaguliwa ili wawahudumie wananchi na ndicho wanachokifanya
Madiwani wa viti maalum wanaounda baraza la madiwani manispaa ya Musoma ni Naima Minga ambaye pia ni Naibu Meya,Asha Muhamed,Amina Masisa,Alieth Kumila na Meryciana Masasi