Home Kitaifa KAYA 15 ZAKOSA MAKAZI ULANGA

KAYA 15 ZAKOSA MAKAZI ULANGA

Jumla ya kaya 15 zimekosa makazi kwasasa katika kata ya Ketaketa wilayani Ulanga kutokana na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha jambo lililopelekea mto Luhombero kujaa maji na kuanza kuvunja nyumba za wananchi waishio pemebezoni mwa mto huo.

Akizungumza baada ya kufika katika eneo hilo Mbunge wa jimbo la Ulanga Mhe. Salim Alaudin Hasham ameiomba Serikali ya kijiji kuwatafutia viwanja mbadala wananchi hao waliopoteza makazi ili wajenge nyumba nyengine na waendelee na maisha yao.

Kwa upande wake mkuu wa Wilaya hiyo Dkt, Julius Ningu amewataka baadhi ya wananchi ambao bado wamesalia pembezoni mwa mto huo kuchukua tahadhari mapema ili kuepusha madhara makubwa kwani bado mvua zinaendelea kunyesha kwa wingi kwa kipindi hiki.

Nao wananchi wa kata ya ketaketa wameshukuru mbunge wa jimbo la Ulanga kwa kuwapatia chakula na mboga ambacho kitawasaidia kwa kipindi cha siku chache hadi pale ambapo watarejea katika hali yao ya kawaida.

Mbunge Salim Alaudin Hasham ametoa mfuko mmoja wa sembe,maharage,chumvi na maturubai kwa kila kaya iliyopata changamoto wakati Serikali ikiendelea kutafuta utatuzi wa haraka wa changamoto hiyo.

Mvua kubwa zinazoendelea kunyesha nchini zimeendelea kuharibu miundombinu mbalimbali jimboni humo ikiwemo barabara,mazao kusombwa na maji na hata makazi kuharibika.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!