Home Kitaifa KATIBU NEC GAVU: VIJANA JITOKEZENI KUGOMBEA NAFASI ZA UONGOZI

KATIBU NEC GAVU: VIJANA JITOKEZENI KUGOMBEA NAFASI ZA UONGOZI

Na Magrethy Katengu–Dar es salaam

Vijana wameshauriwa kuanzia mwaka huu 2024 waache kulalamika hawapewi nafasi za uongozi wajitokeze kuchukua fomu za kugombea nafasi mbalimbali ili wapate kushika hatamu kuongoza nchi yao kwa vyeo mbalimbali ikiwemo Ubunge,udiwani,unyekiti wa serikali za mtaa kwani nao wana mawazo chanya.

Ushauri huo umetolewa Julai 6,2014 Jijini Dar es salaam na Katibu NEC idara ya Organizatio Issa Gavu mara baada ya Uzinduzi wa kampeni ya tunazima zote tunawasha kijani iliyoandaliwa na Umoja wa vijana Uvccm lengo ni kuwandaa vijana na Uchaguzi mkuu ambapo amesema vijana hawana budi kuhamasika kilijenga taifa likiwa na viongozi imara wenye nguvu na mawazo chanya wasioyumbishwa na chochote.

Ukiwa wewe kijana usikae ukazembea fursa hii adhimu ya kuanzia mwaka huu 2024 na kuchagua kugombea kwani nafasi hizi zimeletwa kwa watu wote wenye vigezo sisi tunapenda kuona kuona hawabaki nyuma kwani hatuwezi kupata vijana wazuri nje ya chama cha CCM msizembee” amesema Issa

Gavu amesem CCM inawapa fursa vijana wote kugombe nafasi mbalimbli za uongozi kwani Tanzania ya leo na kesho inaundwa na hilo kundi endapo wataitumia nafasi hiyo vizuri na wakipat nafasi hawana budi kuendeleza amani umoja na Mshikamano ulipo.

“Serikali ilipo madarakani chink ya Usimamizi wa Rais Dkt Samia Suluhu Hassani imekuwa ikiwatengeneza vijana kuanzia kwenye elimu kwani inawapatia mikopo ya elimu ya juu wasome pia imetenga fedha kila halmashauri fungu ili wajikwamue kiuchumi sasa ukisema wewe ni masikini umejitakia hata kama huna ujuzi wowote” amesema Gavu

Kwa Upande wake Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana Chama Cha Mapinduzi UVCCM Taifa Mohamed Kawaida amewataka Vijana kuhakikisha Mikoa yote inazimwa na kuwasha Rangi ya Kijani ili kuunga mkono juhudi mbalimbali anazozifanya Rais Samia katika kulijenga Taifa.

Nae Katibu Mkuu wa UVCCM Taifa Jokate Mwegelo amesema Watahakikisha Uchaguzi Mdogo na Mkubwa unaotarajiwa kufanyika Octobar 2025 unaleta mafanikio na Chama kinashinda Kwa kishindo

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!