Home Kitaifa KATIBU CCM MARA AFUNGUA KAMBI YA MAFUNZO YA VIJANA UVCCM NA KUTOA...

KATIBU CCM MARA AFUNGUA KAMBI YA MAFUNZO YA VIJANA UVCCM NA KUTOA UJUMBE

Na Shomari Binda-Butiama

KATIBU wa Chama cha Mapinduzi ( CCM) mkoa wa Mara Ibrahim Mjanakheri amewataka vijana kujiepusha na wale waotaka kuwatumia vibaya kuvuruga amani ya nchi.

Kauli hiyo ameitoa leo oktoba 4 wilayani Butiama alipokuwa akifungua kambi ya siku 7 ya vijana wa CCM yenye lengo la kuwajenga kimaadili na kuwafanya kuwa wakakamavu.

Amesema katika siku za hivi karibuni wameibuka watu wenye lengo ovu la kutaka kuwatumia vijana kwa masrahi yao binafsi yasiyo na manufaa kwa jamii.

Mjanakheri amesema vijana wasikubali kuwasikiliza watu wa namna hiyo kwa kuwa hawana nia njema kwao na familia zao.

Amesema serikali ya Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan imefanya kazi kubwa ikiwa ni pamoja na kuleta fedha nyingi mkoa wa Mara kwaajili ya miradi ambayo wanapaswa kuitambua

Katibu huyo wa CCM mkoa wa Mara amewataka vijana wanaoshiriki mafunzo hayo kuzingatia nidhamu wakati wote wa mafunzo na baadae kwenda kusemea mazuri yaliyofanywa na serikali.

” Vijana msishawishike na kauli za hao wanaotaka kuchafua amani ya nchi yetu wakataeni na msiwakubalie.

” Yatumieni makambi haya vizuri na kwa lengo lililokusudiwa na kikubwa ni kuzingatia nidhamu wakati wote wa mafunzo mtakapokuwa hapa”,amesema.

Amesema kuelekea uchahuzi wa serikali za mitaa licha ya jukumu la kulinda viongozi na kura CCM vijana wanapaswa kujitokeza kuomba nafasi mbalimbali za uongozi na kushiriki matukio yote ya uchaguzi.

Aidha amewataka vijana hao kuzingatia maadili na kuachana na tabia mbaya ya kujiingiza kwenye ushoga kama wanavyofanya vijana wasiokuwa na maadili.

Katibu wa Jumuiya ya Vijana wa CCM mkoa wa Mara Irene Moleli amesema kambi hilo la vijana ni maamuzi ya sahihi ya kikao cha kamati ya utekelezaji UVCCM mkoa wa Mara.

Amesema kambi lina jumla ya vijana 6000 kutoka wilaya 7 na litakuwa na walimu 17 watakaofundisha mada mbalimbali.

Irene amesema moja ya kazi kubwa ya jumuiya ya vijana ni kuwalinda viongozi wa chama,mikutano ya chama,misafara ya viongozi na kuhakikisha chama kinashinda.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!