Home Kitaifa KATIBU BARAZA LA ARDHI AHUKUMIWA JELA KISA KUOMBA RUSHWA TSH. 20,000

KATIBU BARAZA LA ARDHI AHUKUMIWA JELA KISA KUOMBA RUSHWA TSH. 20,000

News, Njombe.

Mahakama ya wilaya ya Wanging’ombe mkoani Njombe imemhukumu katibu wa baraza la ardhi la kata ya Igwachanya Nuhu Richard Mgaya (28) kulipa faini ya Shilingi 500,000 au kifungo cha miaka mitatu gerezani kwa kosa la kuomba rushwa ya Shilingi 20,000.

Katika kesi hiyo ya jinai namba 18660/2024 ya Jamhuri dhidi ya Nuhu Rishard Mgaya, imeelezwa kuwa mtuhumiwa alishtakiwa kwa kosa la kuomba na kupokea rushwa kinyume cha Kifungu cha 15 (1) (a) na (2) cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (cap 329 Re 2022).

Mahakama imeeleza kuwa mshtakiwa akiwa Katibu wa Baraza la ardhi la Kata ya Igwachanya Halmashauri ya Wilaya ya Wanging’ombe, aliomba kiasi hicho cha fedha kutoka kwa Oberd Willison Mmage na kupokea ili amsaidie kumjazia fomu ya rufaa ya kesi yake aliyotaka kupeleka katika Baraza la ardhi na Makazi la Wilaya huku akijua fomu hiyo hutolewa bure.

Aidha mshtakiwa akiwa mahakamani hapo alikumbushwa mashtaka yake mbele ya Hakimu wa Mahakama ya Wilaya Wanging’ombe James Muhoni, ndipo mahakama hiyo ikamhukumu kulipa faini ya Shilingi 500,000 au kifungo cha miaka mitatu.

Hata hivyo mara baada ya hukumu hiyo kutolewa Mshtakiwa amelipa faini na kuachiwa huru.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!