Home Michezo Kata ya Butimba Yaibuka Kidedea Mashindano ya Polisi Jamii Cup 2023-Mwanza

Kata ya Butimba Yaibuka Kidedea Mashindano ya Polisi Jamii Cup 2023-Mwanza

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi Mkoa wa Mwanza (SACP) Wilbrod Mutafungwa leo Aprili 30, 2023, ameshiriki fainali ya mashindano ya Polisi Jamii Cup 2023 iliyochezwa kwenye uwanja wa Nyamagana jijini Mwanza.

Mechi hiyo ya fainali imeikutanisha timu ya Kata ya Butimba dhidi ya timu ya Kata ya Nyakato zote za jijini Mwanza ambapo timu ya Butimba imeibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Nyakato.

Mshindi wa kwanza katika mashindano hayo yaliyokuwa na Kauli mbiu ya “Chukia Uhalifu Toa Taarifa ya Viashiria vya Uhalifu na Wahalifu ni Wajibu wa kila Mmoja” amejishindia ng’ombe jike mwenye thamani ya TSh. 500,000/=.

Aidha, Mshindi wa pili amepata mbuzi wawili wenye thamani ya TSh. 200,000/= huku mshindi wa tatu akikabidhiwa mbuzi mmoja mwenye thamani ya TSh. 100,000/=.

Washiriki na jamii kwa ujumla tutumie elimu tulioipata kwenye mashindano haya kujifunza na kutoa ushirikiano kwa Jeshi la Polisi utakaosaidia kutokomeza uhalifu kwenye maeneo yetu,” amesema Mutafungwa

Kupitia mashindano hayo Kamanda Mutafungwa alizipongeza timu zilizoshiriki huku washiriki na wapenzi watazamaji wa mpira wakipatiwa elimu ya Polisi Jamii kwa lengo la kuongeza uelewa wa namna ya kupambana na kuzuia uhalifu katika jamii jijini humo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!