Home Biashara KARAFUU YAINGIZA SHILINGI BILIONI 36 MOROGORO

KARAFUU YAINGIZA SHILINGI BILIONI 36 MOROGORO

KATIKA msimu wa 2023 Mkoa wa Morogoro umefanikiwa kuzalisha tani 2,000 za karafuu zenye thamani ya Shilingi bilioni 36.

Hayo yamesemwa na Katibu Tawala wa Mkoa wa Morogoro, Dk. Musa Ally Musa, wakati wa akizungumza na wadau wa mazao ya viungo, ambapo ameweka bayana kuwa tani hizo 2,000 zimezalishwa katika Halmashauri ya Morogoro pekee huku akiweka wazi kwamba umaarufu wa  zao hilo unazidi kuongezeka katika mkoa huo.

Hali ya hewa na ardhi yenye rutuba inatoa fursa ya kuzalisha mazao ya  viungo kwa tija na kwa kukidhi viwango vya kimataifa ambapo mazao ya viungo tunayoyawekea mkazo hivi sasa  ni karafuu, mdalasini (cinnamon), iliki (cardamom), na mchaimchai (lemongrass),” amesema

Amesema zao la karafuu linapenda sehemu zenye miinuko na Mkoa wa Morogoro una sehemu nyingi za aina hiyo, hivyo kuwataka wakulima kuchangamkia fursa hiyo ambayo ina soko la uhakika.

Dk. Mussa amesema ulimaji wa zao hilo  umeanza kuimarika katika Halamshauri ya Wilaya za Morogoro, Kilombero na Mvomero na katika Halmashauri ya Wilaya ya Mlimba.

Mbali ya Mkoa wa Morogoro, jitihada inafanywa ili kilimo cha karafuu kiimarishwe katika Mkoa wa Tanga na Mkoa wa Pwani, hali ya hewa ni sawa na ile ya Zanzibar.

Zanzibar pekee inazalisha tani 4,000 za Karafuu na Zanzibar ni maarufu katika uzalishaji wa Karafuu duniani. Morogoro tayari inazalisha nusu ya karafuu yote inayozaliwa Zanzibar. 

Hii maana yake ni kwamba kuna uwezekano wa Tanzania kuzalisha tani 8,000 ifikapo 2026 kama mikoa ya Morogoro na Tanga itazalisha jumla ya tani 4000 ifikapo mwaka huo,” amesema

Ulimaji wa zao la Karafuu upande wa Bara umetokana utafiti na ushauri wa  Kituo cha Kuendeleza Kilimo Nyanda za Kusini mwa Tanzania (SAGCOT), taasisi inayowashirikisha wadau katika sekta binfasi katika kulima mazao na kuendeleza mnyororo ya thamani ya mazao hayo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!