Home Kitaifa KAMPUNI YA YAS ( ZAMANI TIGO ) YABADILISHA MAISHA YA HUYU DADA...

KAMPUNI YA YAS ( ZAMANI TIGO ) YABADILISHA MAISHA YA HUYU DADA WA KAZI ZA NDANI , APEWA MILIONI 10 … SOMA HAPA USHINDE

Na Mwandishi Wetu.

 Dar es Salaam, 13 Desemba 2024:  Safina Selasi Mgala anayefanya kazi za ndani wa Tegeta jijini ndiye aliyeibuka mshindi wa shilingi milioni 10 katika droo ya tano ya Kampeni ya Magift ya Kugift inayoendeshwa na kampuni ya mtandao wa simu ya Yas Tanzania.

Kufuatia ushindi Safina alikabidhiwa mfano wa hundi na kisha kuingiziwa kiasi hiyo cha pesa kwenye simu yake kupitia Mixx By Yas (zamani Tigo Pesa) katika hafla hiyo iliyofanyika Tegeta Nyuki jijini na kushuhudiwa na umati ulifurika eneo hilo.

Safina alijishindia kiasi hicho cha pesa kutokana na kutumia huduma za Yas ikiwemo kununua vocha, kufanya miamala mbalimbali kupitia Mixx By Yas ikiwemo malipo ya huduma za serikali, ikiwemo kulipa bili za maji, umeme, kutuma na kupokea pesa na huduma nyinginezo.

Kwa ushindi wa Safina jamii inajifunza kuwa ushindi katika kampeni ya Magift ya Kugift unaweza kumfikia mtu yeyote unachotakiwa ni kufanya juhudi kutumia huduma za Yas aliongezea kuwa pesa iyo ataitumia kufungua biashara ya Nguo.

Kwa upande mwingine Makao Makuu ya Kampuni ya Yas , Zawadi mbalimbali za Fedha na Simu zilizotelewa ambapo Watumiaji wa mtandao wa simu wa Yas kupitia Kampeni yake inayoendelea ya Magift ya Kugift droo ya tano washindi watatu wamejinyakulia shilingi milioni moja kila mmoja.Washindi hao walikabidhiwa hundi ya fedha walizojishindia na msemaji wa kampeni hiyo, Haji Manara maarufu kama Bugati.

Kuwakabidhi washindi hao zawadi zao Bugati aliwataka watumiaji wengine wa simu kutumia mtandao wa Yas kwa ajili ya huduma mbalimbali kama vile kufanya miamala mbalimbali kama vile kuweka na kutoa pesa, kufanya malipo mbalimbali kwa kutumia Mixx By Yas zamani Tigo Pesa.Ameendelea kusema kuwa kwa kufanya hivyo unakuwa umeingia kwenye droo hiyo na hivyo kuweza kuondoka na zawadi mbalimbali kama vile simu janja, pesa taslimu shilingi milioni moja au kumi na kufurahia vyema kipindi hiki cha sikuu za Krismas na Mwaka mpya.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!