Home Kitaifa Kampuni ya Seed -co yaja na Majibu ya Mkulima kuhusu ulimaji Bora...

Kampuni ya Seed -co yaja na Majibu ya Mkulima kuhusu ulimaji Bora na Wenye Faida

Kampuni ya seed- co imewataka wakulima kutembelea mabanda yao katika maonyesho ya nanenane yanayoendelea nyamhongoro Jijini mwanza.

Akizungumza Ayubu juma Bisaga bwana shamba na Afisa masoko wa Mwanza, Geita na Musoma, amesema kuwa mbegu alizonazo zinaweza kumkwamua mkulima kwani niza muda mfupi kuanzia siku sabini na Tano(75) na zinavumilia ukame.

Ameongeza kwa kusema mbegu hiyo ya chapa tumbili kama mkulima ataipanda kwa kuzingatia kanuni za kilimo Bora ambazo ni senti mita 45 Kwa mstari na mstari na senti mita 30 kutoka shina na shina anaweza kupata mazao mengi na mazuri kuanzia junia 48 na kuendelea.

Naye bibi shamba, Venitha Domitian amewataka vijana kujikita kwenye kilimo cha mbogamboga ili waweze kujikwamua kiuchumi kwani kuna mazao yanaiva ndani ya miezi mitatu mazao hayo ni
kama nyanya inayoitwa mkombozi F1, inavumilia sana ukame na magonjwa ya mnyauko

Lakini pia nyanya hiyo inavumilia sana ukame hasa Kanda ya ziwa ambapo kuna tatizo la unyauko na ukame hivyo basi Seed-co wamekuja na suluhisho na tatizo la ukame.

Pia ameeleza kuchangamkia fursa Kwa vijana na watanzania wote kwani ameeleza kuwa wao wanatoa elimu kwa vitendo ili kuwasaidia watanzania kulima kilimo chenye tija na kuweza kujikwamua kiuchumi na si kubaki wanatangatanga mitaani.

Maafisa hao wameeleza kuwa wakulima kulima kwa kuzingatia huduma nyingine za shamba kama vile matumizi mazuri ya mbolea, viatilifu na kuvuna Kwa wakati mkulima anaweza kupata mazao mengi.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!