Home Kitaifa KAMPUNI YA GF TRUCKS & EQUIPMENT LTD YAINGIA MAKUBALIANO YA UDHAMINI NA...

KAMPUNI YA GF TRUCKS & EQUIPMENT LTD YAINGIA MAKUBALIANO YA UDHAMINI NA GEITA GOLD FC

Na mwandishi wetu

GF Trucks & Equipment LTD ni kampuni ya uuzaji wa Magari Makubwa (FAW), Machine(XCMG) na spare parts yatangaza kuingia Udhamini na Geita Gold FC wenye lengo la kuinua vipaji, ajira kwa vijana na kuimarisha michezo Tanzania pia kuimarisha ushirikiano wa wana Geita katika biashara.

Akizungumzia makubaliano hayo mara baada ya utiaji saini huo uliofanyika ofisi ya GF Trucks & Equipment LTD Vingunguti, jijini Dar es Salaam, Meneja Masoko na Mawasiliano wa GF Trucks & Equipments LTD Bw. Smart Deus amesema kuwa, Lengo mahususi ni kuimarisha ushirikiano na kuunga mkono juhudi za Geita Gold FC.

GF Trucks & Equipment LTD wamekuwa wadau wakubwa kwenve michezo, Afya, miundombinu pamoja kuunga mkono serikali ya awamu ya sita chini ya Mh Rais Mama Samia Hassan Suluhu. Kupitia unadhamini huu unalenga kusaidia timu ambayo ina vijana wanaopata ajira, wana jenga afya na kuleta ushindani kwenye michezo.

GF Trucks & Equipment LTD imetoa pongezi kubwa kwa Geita Gold FC kwa kufanya vizuri kwenye ligi kuu ya Tanzania na kupata nafasi kushiriki michuano ya kimataifa. Akizungumza Bw Salman Karmali Afisa MkUu wa Biashara.

Leo wameingia makubaliano kwa lego kuendeleza mashirikiano baina GF Trucks & Equipment LTD na wadau hasa zaidi Gita Gold FC ikiwa ni timu inayotekea Mkoa Gita ambapo biashara kubwa kwao ni uchimbaji madini, wanakuwa washirika wakubwa kibiashara na jamii kwa ujumla.

Lengo letu ni kuhakikisha kuwa tundendelea kuwa wauzaji na watoaji wa huduma bora wa Magari Makubwa(FAW) na Machine (XCMG) ili kuyafikia” Alisema Salman Karmali

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!