Home Kitaifa KAMPENI YA TBS ELIMU KWA UMMA KUTIKISA WILAYA ZA MKOA WA ARUSHA

KAMPENI YA TBS ELIMU KWA UMMA KUTIKISA WILAYA ZA MKOA WA ARUSHA

 Na Adery Masta.

Shirika la Viwango Tanzania (TBS) linaendelea na Kampeni yake Ya kutoa Elimu Kwa Umma katika Ngazi za Wilaya ambapo hadi sasa Shirika hilo limetoa Elimu Kwa wananchi Wafanyabiashara na Wajasiriamali Wadogo Ndani ya Wilaya 93 nchi nzima na Lengo likiwa ni kuzifikia Wilaya Zote nchini. 

Meneja Wa Uhusiano na Masoko TBS Bi.  Gladness Kaseka ( kushoto ) akizungumza na Mwakilishi wa Kikundi cha akina Mama wasindikaji wa Maziwa Wilayani Karatu ( kulia ) kuhusu hatua za kufuata ili kuweza kupata alama ya ubora ya TBS ambayo inatolewa BURE kwa wajasiriamali wadogo , katikati ni Bi. Neema Mtemvu , Eliud Mwasyebule ( kutoka TBS ) na Mercy Dawasa – Afisa Maendeleo ya Jamii – Karatu.

Akizungumza hivi karibuni katika Wilayani Karatu mkoani Arusha Meneja Wa Uhusiano na Masoko TBS Bi.  Gladness Kaseka amesema lengo la Shirika hilo ni kutoa Elimu Kwa Umma katika Ngazi za Wilaya zote.

” Kwa sasa TBS tumeamua kuwafikia Wajasiriamali ,Wafanyabiashara na wananchi katika Ngazi Za Wilaya ili  kuwapatia utaratibu unaotakiwa kwa ajili ya kupata alama ya Ubora, kusajili majengo ya Biashara ya chakula na Vipodozi ili kuepuka Usumbufu unaoweza kujitokeza, umuhimu wa kununua bidhaa zenye ubora  na namna ya kuwasiliana na TBS wapatapo changamoto yeyote. Elimu hii ya Umma ipo katika ngazi ya Wilaya na hadi sasa TBS imezifikia Wilaya 93, na kwa hapa Arusha tutatoa Elimu katika wilaya za Karatu, Loliondo – Ngorongoro, Longido , Monduli na Arusha yenyewe “. amesema Bi.  Kaseka 

Aidha Bi. Kaseka amewasihi Wananchi kuhakikisha  wanasoma taarifa zinazopatikana katifa vifungashio za bidhaa pamoja na muda wa mwisho wa matumizi na kununua bidhaa zilizothibitishwa ubora wake na TBS ili kuepuka hasara ya kupoteza pesa na kulinda afya zao. 

Hapo awali wakizungumza kwa nyakati tofauti na Vikundi vya Wajasiriamali wanaosindika maziwa na Wanaooka mikate Wilayani Karatu, TBS wameweza kuwapatia utaratibu wa jinsi ya kupata alama ya Ubora ambayo inatolewa Bure, alama itakayowasaidia si tu kukuza Biashara zao , Bali pia kulinda afya za Wateja wao. 

Wakizungumza kwa nyakati tofauti tofauti Bi. Hoisa Monyo – Katibu wa Kikundi kinachojishughulisha na Usindikaji wa Maziwa na Bi. Matilda Shirima – Katibu wa Kikundi cha Uokaji Mikate, wamelipongeza Shirika la Viwango Tanzania ( TBS ) kwa Elimu waliyoamua kutoa kwa maana imewafumbua Mambo mengi kuhusu umuhimu wa Viwango katika bidhaa wanazozizalisha.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!