Home Kitaifa KAMPENI YA SMAUJATA KUFIKA KILA ENEO MKOANI MOROGORO.

KAMPENI YA SMAUJATA KUFIKA KILA ENEO MKOANI MOROGORO.

Na, Saidi Ibada, Morogoro.

Kampeni ya Shujaa wa Maendeleo na Ustawi wa Jamii Tanzania (SMAUJATA) Mkoani Morogoro imedhamiria kuwafikia Wananchi Kutokana maeneo mbalimbali mathalani wale wanaoishi maeneo ya vijijini ili kutoa elimu ya namna ya kuibua na kupinga ukatili na unyanyasaji wa kijinsia unaoikumba jamii hapa Nchini.

Akizungumzia mikakati ya SMAUJATA Morogoro mjini katika kikao kilichowaleta pamoja wanachama hao, Mwenyekiti wa kampeni hiyo Bw. Musa Bulima alisema katika utekelezaji wa kampeni hiyo iliyo chini ya wizara ya maendeleo ya jamii, jinsi, wanawake na Makundi maaalum, imedhamiria kuibadilisha jamii iondokane na ukatili wa kijinsia.

Bulima alisema kuwa wao kama wanaharakati wataufikia mkoa wa Morogoro kuanzia ngazi ya Halmshauri , kata, vitongoji hadi vijiji na mitaa ili kutoa elimu na misaada mbalimbali ya namna ya kukabiliana ukatili wa kijinsi ili kulifanya taifa la Tanzania kuwa endelevu
katika Nyanja zote za kijamiii na kiuchumi.

“Mipango kazi ipo, kampeni zimeanza kwa baadhi ya kata Morogoro mjini. Tunadhamiria kutoa elimu kwenye jamii kwa kuanzia ngazi ya familia, vikindi vya akinamama, bodaboda pamoja na vituo vya kulelea watoto yatima. Tumeanza na makundi ya akinamama, pia tumejipanga kutumia makongamano mbalimbali ili kuwafikia wadau na kutoa elimu” alisema.

Aliongeza kwa kusema kuwa ofisi ya afisa ustawi wa jamii mkoani Morogoro imewaelekeza wanaharakati hao kufika hadi ngazi za halmashauri na vijiji kutoa elimu ya kuukomesha ukatili katika jamii ambapo pamoja na mambo mengine alishukuru uwepo wa dawati la jinsia kwani litawasaidia katika kupata mwongozo wa namna ya kuifikia jamii katika kufanikisha lengo la SMAUJATA.

“Nashukuru kuwa tunafanya kazi pamoja nanyi, ambao mnauzoefu katika utetezi wa haki za watu wa jinsia mbalimbali na naamini mtatu kuwa mmtatoa muongozo sahihi ili kutokomeza ukatili. Tangu kampeni hii izinduliwe Juni 16, wilayani Mvomero. Mpaka Sasa kesi 6 zipo kwenye dawati na zinashughulikiwa. ” alisema

Aidha, ametoa wito kwa Wananchi kote Nchini kushirikiana na SMAUJATA kwa kuwaibui wote wanaotenda ukatili wa kijinsia ili Sheria ichukue mkondo wake na hatimaye kukomesha ukatili wa kijinsia kwa kutoa taarifa kuwezesha utekelezaji wa kampeni ya kupinga ukatilii.

“Wanajamiii wanatakiwa kutoa taarifa za matendo maovu yanayoendelea katika nyumba zao, shuleni na maeneo yote ambayo watu wanakumbana na kaadhia ya unyanyasaji na ukatili kwa kupiga namba 116 na atapata msaada, Pia watu wajitolee katika kufanikisha kampeni hii, kampeni ambayo tunatakiwa kuona tumeumia na kunyanysika vya kutosha na kufikia hatua ya kuwa lazima tukatae unyanyasaji,dawa ya jipu ni kulitimbua, taarifa zikitufikia sisi tutahakikisha mhusika anachukuliwa hatua stahiki”. Alisema Bulima.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!