Home Kitaifa KAMATI YA VIJANA WAZALENDO KUJADILI SERA YA TAIFA YA MAENDELEO YA VIJANA...

KAMATI YA VIJANA WAZALENDO KUJADILI SERA YA TAIFA YA MAENDELEO YA VIJANA KWA MAKONGAMANO NCHI NZIMA

Mikoa kumi kufikishiwa mahudhui ya sera ya taifa ya maendeleo ya vijana (2007) toleo la mwaka 2024 kwa awamu ya kwanza kupitia kamati ya vijana Wazalendo lengo likiwa ni kundi la vijana linufaike na fursa mbalimbali zilizopo katika taifa.

Hayo yamesemwa na Mratibu wa Kamati ya vijana Wazalendo Omary Punzi akizungumza na Waandishi wa Habari wakati akitambulisha ratiba ya makongamano hayo ya vijana kwaajili ya kutoa elimu ya sera ya taifa ya maendeleo ya vijana (2007) toleo la mwaka 2024 huko mjini Kibaha mkoani Pwani.

Alisema kamati hiyo ya vijana Wazalendo imepata kibali kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi vijana, ajira na walemavu kupitia Waziri Ridhiwani Kikwete kuhakikisha inatafsiri sera hiyo kwa vijana nchini kwa kutumia makongamano mbalimbali hata kufikia vijana nchi nzima.

Punzi alisema ratiba ya Kamati hiyo itaanzia katika mkoa wa Pwani katika Halmashauri zake tatu za Rufiji, Bagamoyo na Chalinze kisha mkoa wa Dar es salaam, Morogoro, Tanga, Arusha, Kilimanjaro, Mbeya, Dodoma, Iringa na Mwanza.

Aliwataka vijana kujitokeza kwa wingi katika matukio ya makongamano hayo ili wasikie kisha waweze kuchukua hatua wekulingana na elimu watakayoipata ili wanufaike na fursa mbalimbali zilizopo katika taifa letu.

Aidha ameomba Wadau mbalimbali wa masuala ya maendeleo ya vijana kuunga mkono kwa Hali na Mali jitihada hizo za Kamati ya vijana Wazalendo ili kuhakikisha vijana wote wa Tanzania wanapata uelewa wa sera hiyo ya taifa ya maendeleo ya vijana (2007) toleo la mwaka 2024.

Punzi alitaja baadhi ya sera zitakazofafanuliwa kwenye makongamano hayo kuwa ni pamoja na kuelekea Baraza la vijana taifa, sera ya utoaji wa mikopo ya asilimia kumi kwa vijana na mikopo inayotolewa na sekta zingine kwa kundi la vijana nchini, sera ya matumizi ya nishati safi kwa vijana ikiwa ni pamoja na kuangalia jinsi ambavyo sera inavyoelekeza namna vijana wanatakiwa kuitunza amani ya nchi.

Mwenyekiti wa Kamati ya vijana Wazalendo Farida Kongoi alisema kuundwa kwa sera ya taifa ya maendeleo ya vijana lengo lilikuwa ni vijana wapate mwongozo wa kuendana na masuala ya siasa na kijamii ikiwa ni pamoja na mwelekeo wa kiteknolojia kwa mwongozo wa sera ya nchi.f

Mwanasheria wa Kamati ya vijana Wazalendo Godfrey Kizito amesema pia vijana watafafanuliwa kuhusu Sheria zinazohusu haki na masuala ya vijana.

Aidha Kizito alisema tatizo kubwa lililopo katika Sheria zilizopo katika sera vijana hawazifahamu Hilo ndio lengo la wao Kamati ya vijana Wazalendo kuzunguka nchi nzima kutoa elimu hiyo kwa vijana hasa ikizingatiwa kuwepo kwa changamoto ya lugha iliyotumika kuandika sheria zetu nchini kuwa ni Moja ya kikwazo cha vijana kuzielewa.

Naye Mkurugenzi wa Great leaders organization na Mratibu na Mwandaaji wa kongamano la Wazazi na Walezi nchini Dubai Dkt. Debora Nyamlundwa alisema katika kongamano hilo Kuna kujifinza fursa mbalimbali zilizopo katika taifa hilo kuja kuendeleza hapa nchini

Alisema katika kongamano hilo nchini Dubai litaonyesha fursa mbalimbali ambazo anatamani ziletwe hapa nchini zinufaishe vijana.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!