Na Boniface Gideon, TANGA.
KAMATI ya Siasa ya Chama cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Tanga ikiongozwa na Mwenyekiti wake Rajab Abdurhamani imeonesha kukerwa na kitendo cha baadhi ya miradi kusuasua huku baadhi ya miradi ikikumbwa na masakata ya wizi wa vifaa.
katika Hospitali ya wilaya aya Pangani Mkoani Tanga kumekumbwa na sakata la wizi wa vifaa ambapo misumari gunia mbili iliibiwa hivi karibuni .
Kamati hiyo imetoa maagizo kwa vyombo vya usalama hususani Jeshi la Polisi kufanya uchunguzi na watakaowabaini walihusika kwenye tukio hilo hatua kali za kisheria zichukuliwe.
Hayo yalibainika leo wakati wa ziara ya kamati ya siasa yakukagua miradi wilayani hapa iliyokuwa na lengo la kufuatilia maagizo yake yaliyotolewa wakati wa ziara yake ya hivi karibuni ambapo .
Mwenyekiti wa ccm mkoa wa Tanga Abdalrahman alisema pamoja na hayo wachukuliwe hatua za kinidhamu na asionewe mtu huku akisisitiza aliyetia mkono wake kuiba vifaa hivyo ashughulikiwe.
Akiwa Hospitalini hapo baada ya kukagua ukarabati wa Hospitali hiyo ambao unagharimu milioni 900 ndipo alipoelezwa wizi huo na Mkuu wa wilaya ya Pangani Zainabu Abdallah wakati akipopata nafasi ya kuzungumza.
Mwenyekiti huyo alisema lazima washughulikiwe kwa kuchukuliwa hatua kali ili iweze fundishwa kwa watu wengine wenye tabia za namna hivyo maanaa zikivumiliwa vitakwamisha juhudi za kimaendeleo ambazo zinafanywa na Serikali.
“Kwa maana tutawapa lawama ndugu zetu waliopewa nafasi ya kusimamia miradi ikiwemo Mkurugenzi na Mkuu wa wilaya na katika hili nikutake Mkuu wa wilaya usicheke na mtu na ukiacha hilo ninazo taarifa nyegine nimeweka watu wangu nitakapozithibitisha nitachukua hatua kuna vifaa viliibwa hapa hospitali lakini jana usiku baada ya kusikia ninakuja vimerudishwa watu hawaogopi wala hawana haya hilo halikubaliki” alisema
Mwenyekiti huyo pia aliwapongeza uongozi wa Hospitali hiyo kwa kusimamia mradi huo wa ujenzi wa Hospitali huku akionyesha kuridhika nao kwa kiasi kikubwa kwa sababu thamani ya fedhana kinachoonekana kinaendana.
“Niwaombe wananchi wenzangu lazima tumhurumie Rais Wetu Dkt. Samia Suluhu kwa maana anahangaika usiku na mchana muda wowote siku zote halali kwa sababu ya kuwasaidia Watanzania kuwaondolea adha zinazowakabili pia mbunge wetu anapambana sana kujenga hoja kwamba hospitali yetu na hapa Hospitalini ameleta Milioni 900 kwa ajili ya ukarabati hivyo tusiwakatishe tamaa viongozi wetu” Alisema
Aidha alisema kwa maana wakati miradi inapotekelezwa zinatumika fedha nyingi ambazo zimeletwa kwenye wilaya yenu katika utekelezaji wa miradi hiyo lazima wananchi wawe waaminifu ili lengo liweze kutimia lakini inapojitokeza watu wanaiba misumari inakwamisha juhudi hizo.
Hata hivyo aliwataka viongozi wa wilaya hiyo kuendelea kuwa wabunifu katika maeneo yao ikiwemo kuendelea kumuunga mkono Rais Dkt Samia Suluhu anayejali matatizo ya wananchi anaowaongoza.
Mwenyekiti huyo aliwataka wananachi hao kuhakikisha mwaka 2025 hawana Rais mwengine zaidi ya Dkt Samia Suluhu mambo anayoyafanya ni makubwa ya kimaendeleo watapata muda kwenda kuyaelezea.
Awali akizungumza katika ziara hiyo Mkuu wa wilaya ya Pangani Zainabu Abdallah alimueleza Mwenyekiti huyo kwamba Serikali ya Rais Dkt Samia Suluhu aliwapelekea million 900 kwa ajili ya ukarabati wa Hospitali ya wilaya hiyo huku akieleza wakati anapofanya ziara na kamati ya usalama kukagua ujenzi huo ndipo walipobaini uwepo wa wizi huo.
Alisema baada ya kulibaini hilo alimuelekeza Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya wilaya hiyo (DMO) aweze kuchukua hatua kutokana na kupotea magunia mawili ya misumari lakini hawakuripoti katika Jeshi la Polisi ili uchunguzi ufanyie na hatua zichukuliwe.
“Lakini nilitoa maelekezo kwa DMO achukue hatua ili sheria ichukue mkono wake lakini niliwataka lega ya vifaa vyote vinavyongia na kutoka vya zamani na vipya na hali yake ipoje bahati nzuri DMO aliniandikia taarifa na nilimueleza aende kufungua kesi na kesi tayari imeshafunguliwa kituo cha Polisi na uchunguzi unaendelea na hivi vilipotea wakati wanahamisha vifaa kutoka sehemu waliokuwa wamehifadhi kwenye stoo mpya” Alisema
Mwisho