Home Kitaifa KAMATI YA BUNGE YAKUBALIANA NA MIRADI YA NHC, YAMPONGEZA RAIS SAMIA

KAMATI YA BUNGE YAKUBALIANA NA MIRADI YA NHC, YAMPONGEZA RAIS SAMIA

KAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeridhishwa na utekelezaji wa miradi inayosimamiwa na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) na imepongeza hatua ya Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kutoa fedha kwa ajili ya kuendeleza miradi iliyokuwa imesimama.

Hayo yamesemwa Juni 30,2024 na Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Timotheo Mzava wakati akizungumza na waandishi wa Habari mara baada ya kumaliza ziara ya kukagua miradi mitatu inayotekelezwa na Shirika ikiwemo wa Samia Housing Scheme (SHS), mradi wa Kawe711 na Morocco Square ambayo yote iko Jijini Dar es Salaam.

Aidha Mhe. Mzava amesema kuwa uamuzi wa Rais Samia kutoa kibali kwa NHC kuendelea na utekelezaji wa miradi yake ni wakizalendo na kwamba NHC kwa sasa hawana kisingizo cha kutokamilisha miradi hiyo kwa wakati.

kazi hii isingefanyika vizuri kama siyo nia, moyo, mtazamo na maono ya Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan hasa kutoa kibali kwa NHC kuendelea na utekelezaji wa miradi hiyo, NHC kwa sasa hawana kisingizo tena cha kutokamilisha miradi hii kwani tayari fedha zimeshatolewa”amesema Mhe. Mzava.

Kwa upande wake Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Geophrey Pinda amesema kuwa miradi hiyo ipo katika hatua nzuri na kwamba mradi wa Morocco Square umeshakamilika kwa asilimia 99 na tayari majengo yaliyopo yameshachukuliwa na wapangaji na wanunuzi kwa asilimia 90, nakwamba hiyo ni ishara kuwa miradi hiyo sasa inafanya vizuri.

Aidha ameishukuru kamati ya Bunge kwa ushauri inayoutoa kwa wizara kuwa umeisaidia wizara na taasisi zake kuboresha shughuli zake na kuahidi kuendelea kuisimamia maelekezo ya Mhe. Rais kuakikisha miradi hii inamalizika kwa wakati

Naye Mkurugenzi Mkuu wa NHC Ahmed Abdallah Ahmed, amesema kuwa hadi sasa katika nyumba za makazi na biashara zilizouzwa, Shirika limekusanya kiasi cha Sh.Bilioni 30 na kiasi cha Sh.Bilioni 35.9 kinaendelea kukusanywa huku eneo la maduka limeshapangishwa kwa asilimia 98 ambapo kwasasa upangaji wa bidhaa unaendelea ili kufungua maduka hayo mwezi Julai mwaka huu.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!