Kamati ya Amani Mkoa wa Mwanza imekutana na kulaani na kupinga tukio la kanisa katoliki kuvamiwa na kuharibiwa kwa baadhi ya vifaa mkoani Geita na kuliita tukio hilo kuwa la uvunjifu wa amani na kuiomba serikali kuhakikisha sheria inafuata mkondo wake.
Mwenyekiti Mwenza wa kamati ya amani Mkoa wa Mwanza Hassan Kabeke amesema, tukio hilo limeleta simanzi kubwa kwa kufanya matendo machafu kwa kuvunja vitu hivyo sie kama kamati ya amani mkoa wa Mwanza tunatoa pole sana kwa tukio hilo lililotokea.
‘’Nitumie nafasi hii kufikisha salamu za mheshimiwa muft na sheikh mkuu wa Tanzania Dkt Sheikh Abubakari Bin Zuber Bin Ally mimi nikiwa sheikh wa mkoa wa Mwanza nimwakilishi wake amenitaka na kuniomba nifikishe salamu zake kuwa jambo ilo amelipokea kwa masikitiko makubwa akiamini Tanzania inaendeshwa kwa mujibu wa katiba,” – Hassan Kabeke Sheikh wa mkoa wa Mwanza.