Home Kitaifa Kamanda Mutafungwa akemea vitendo vya wananchi kujichukulia sheria mkononi

Kamanda Mutafungwa akemea vitendo vya wananchi kujichukulia sheria mkononi

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Wilbroad Mutafungwa ametoa elimu ya namna ya kuzuia uhalifu na kuacha kujichukulia sheria mkononi kwa wananchi wa kata ya Bukokwa, Halmashauri ya wilaya ya Buchosa Mkoani humo.

Elimu hiyo imetolewa Septemba 20,2023 wakati Kamanda Mutafungwa alipokuwa akizungumuza na wakazi wa Kata na Wananchi wa Buchosa ikiwa ni mwendelezo wa ziara zake za kutoa elimu kwa wananchi juu ya kujiepusha na vitendo vya uhalifu ikiwemo ubakaji, ulawiti sambamba na vitendo vya ukatili wa kijinsia.

Sambamba na hayo, Kamanda Mutafungwa amekemea vitendo vya baadhi ya watu kujichukulia sheria mkononi kwa watu wanaotuhumiwa kuhusika kwenye makosa mbalimbali na kuwaeleza Wananchi kuwa vitendo hivyo havikubaliki na hatua kali za kisheria zitaendelea kuchukuliwa dhidi ya wanaojichukulia Sheria mkononi.

Wananchi kuweni makini., acheni kujichukulia Sheria mkononi. Acheni vyombo vya dola vifanye kazi yake”, amesema Mutafungwa.

Aidha, Kamanda Mutafungwa amesema mkakati wa Jeshi la Polisi ni kuzuia uhalifu kwa kushirikisha jamii husika katika eneo husika kutoa taarifa moja kwa moja ili kuwabaini watu wanaofanya vitendo hivyo ndani ya jamii.

Mutafungwa amesema kauli mbiu ya Polisi Jamii inasema “Polisi jamii Kwa usalama na maendeleo yetu”., hivyo tukishirikisha na jamii matukio haya yatakoma na jamii itakuwa salama.

Kwa upande wake, Mkuu wa Polisi wilaya ya Sengerema., Mrakibu Mwandamizi wa Polisi (SSP) Mohammed Haji amesema kuwa, mwaka 2023 matukio ya ukatili yaliyoripotiwa vituo vya Polisi kwa wilaya ya Sengerema mwaka 2022 ni 245 huku mwaka 2023 yameripotiwa matukio 169 ikiwa ni tofauti ya matukio 79 ndani ya miaka miwili.

Aidha, Tabu Mazige mkazi wa Bukokwa, akizungumza kwa niaba ya Wananchi., amesema kuwa mkakati wa Jeshi la Polisi wa kushirikisha jamii katika masuala mazima ya kuzuia vitendo vya kiharifu itasaidia kukomesha vitendo hivyo hususani kwa watoto ambao wamekuwa wakikumbwa na changamoto hiyo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!